![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo (kushoto) Nsolo Mlozi akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa NIC Yessaya Mwakifulefule (Kulia) |
Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia
Akson, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za Capital City Marathon Dodoma , itakayo fanyika October 10 mwaka huu katika chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.
Capital City Marathon kwa mara ya kwanza ilisajiliwa rasmi mwaka 2019. Mbio hiyo kwa mara ya kwanza ilikimbiwa Julai 7,2019 ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na wakimbiaji 1600 ikiwa ni moja ya mbio iliyofanya vizuri wakati huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini hapa,
MKurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo , Nsolo Mlozi amesema wameona ni bora
kuendeleza adhma ya mbio hizo ili
kudumisha michezo pamoja na kujenga afya.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo Nsolo Mlozi |
‘’Jiji la Dodoma limepata wageni wengi waliohamia ,muda
unapatikana mwingi sana jioni tunapotoka ofisini, kwahiyo tukaona tuboreshe
urafiki wetu na undugu wetu katika michezo ,sambamba na hayo tumekuwa
tukifanya shughuli mbalimbali ikiwemo mbio za michezo kwa kila mwezi ,leo rasmi
tunatangaza tarehe 10/10/2021 tutafanya mbio yetu ya pili kubwa ambayo inaitwa
Second City Marathon ambayo itafanyika katika chuo kikuu cha Dodoma ‘’ amesema
Naye Yessaya Mwakifulefule, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma
kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC) ,amesema wana furaha ya kushirikiana
na Capital City Marathon kwa kudhamini mbio hizo .
![]() |
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule |
‘’Sisi kama NIC tunaamini kuwa marathon hizi ni chanzo cha
ajira kwa vijana wengi ,tunaona ndugu zetu wakenya wanafanya vizuri katika eneo
hilo lakini kabla ya hapo tulikuwa
tukitamba miaka ya nyuma Tanzania halafu kidogo vijapi vikapotea ‘’ amesema
Wakati huo huo Mwakifulefule Amesema, wameona ni bora (NIC) wakashirikiana
na waandaaji wa mbio hizo kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo‘’ lakini
kuwahamasisha vijana kujiunga na mbio hizo na kuweza kushinda , lakini pia
kufikisha Taifa katika mbio za kimataifa’’
Kwa upande wake Robert Mabonye Katibu wa Chama cha Riadha
Mkoa wa Dodoma, amewasisitiza wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kuhudhuria
katika mbio hizo ‘’ Niwaambie wakazi wa Dodoma hii ni fursa wajitokeze kwa
wingi sisi Dodoma tuwe wakwanza kuchukua donge nono iliyotolewa na Capital City
Marathon’’
Mwisho.
Comments
Post a Comment