Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akimwonesha aina ya dawa za moyo alizomwandikia  mkazi wa Kigamboni wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na  wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya wilaya ya Kigamboni   ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani



Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa  akiangalia picha inayoonesha mlo kamili wakati Afisa lishe wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Husna Faraji alipokuwa akimwelezea kuhusu lishe bora wakati wa  upimaji wa magonjwa ya Moyo uliofanywa na  wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani


Mtafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina  Komba akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa jinsi wanavyowapima  na kupata uwiano wa urefu na uzito wananchi waliofika katika Hospitali ya wilaya hiyo wakati wa  upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na  wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akimsikiliza Alex Kyando kutoka kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Ajanta Pharma Limited alipokuwa akimweleza kuhusu aina ya dawa za moyo wanazozitoa  kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa na  wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.