WAHANDISI 630 KULA KIAPO CHA UTII

Na. Rhoda Simba, DODOMA 

JUMUIYA ya wahandisi Tanzania inatarajia kuadhimisha siku ya wahandisi ambapo jumla ya wahandisi wataalamu 630 watakula kiapo cha utii ili kuhakikisha kuwa wahandisi wanawajibika vyema kwenye taaluma zao. 

 


Maadhimisho hayo yataadhimishwa Septemba 2 hadi 3 mwaka huu jijini Dodoma ambapo wahandisi hao watakula kiapo cha utii hali itakayoongeza uwajibikaji katika maamuzi yao na utendaji kazi wao wa kihandisi wa siku hadi siku. 

Akiongea leo jijini hapa na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano Mkuu wa Bodi ya Usajili wahandisi nchini (ERB) Profesa Bakari Mwinyiwiwa amesema lengo kubwa la kuadhimisha siku ya wahandisi ni kuiwezesha jumuiya ya kihandisi na kuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi.

"Shughuli zitakazo fanywa  wakati wa kuadhimisha siku ya wahandisi pamoja na kongamano la wahandisi vijana, majadiliano ya kitaaluma, kiapo cha wahandisi wataalam, maonesho mbalimbali ya ubunifu, teknoljia na biashara, kutoa tuzo mbalimbali kwa wahandisi na makampuni yaliyoshamiri kwenye sekta ya uhandisi pamoja na kuwatambua  na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwaka  wa mwisho (2019,2020)" amesema Profesa Mwinyiwiwa

Amesema maadhimisho hayo ni Makubwa na yatahudhuriwa na idadi kubwa ya watu ambapo bodi imewaalika viongozi wa ngazi za juu serikalini, mashirika ya umma na binafsi, wageni kutoka nchi za njee,wahandisi,makandarasi,wasanifu na wabunifu majenzi,wanafunzi wanaosomea uhandisi,na wadau mbali mbali.

Amesema kuwa wageni watakaoshiriki ni kutoka nchi za Uganda,Misri,na wengine watashiriki kwa njia ya mtandao kutoka afrika kusini, DRC, Rwanda, Botswana, na Kenya.

Siku ya wahandisi ni siku ya pekee kwa wahandisi wa Tanzania kuweza kuonesha yale wanayoweza kufanya kwa maendeleo ya nchi, ambapo siku hiyo ikitumika vizuri inaweza kuzidisha kasi ya maendeleo nchini hapa.

 

Mwisho

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.