Na Rhoda Simba, Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa Sh. Bilion 1.3 kwaajili ya kumalizia mtambo wa usambazaji maji katika mradi wa Iyumbu.
Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipotembelea na kukagua mradi wa maji wa Iyumbu na Nyumba 300.
"Mradi huu ulikuwa unagharimu sh. Bilion 2.7 na katika awamu ya kwanza Rais Samia ametoa Bilion 1.4 na Fedha inayobaki itakamilishwa hivi karibuni" amesema Aweso
Kadhalika kwa mamlaka aliyopewa
na Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo aliyekuwa Meneja Ufundi Duwasa
Mayunga Kashilimu kuwa Mkurugenzi huku Mhandisi James Ryoba aliyekuwa
akijitolea kuagiza ajiriwe .
" Katika awamu ya kwanza Serikali iliahidi kuwa mradi huu ulipangwa kutekelezwa kwa kiwango cha Fedha cha bilioni2.7 na serikali kwa awamu ya kwanza ilitoa bilioni 1.4"amesema Aweso
Katika hatua nyingine, Aweso ametuma salamu kwa wahandisi Wa Wizara kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwani wapo watalaamu wengi wamemaliza vyuo na wapo mtaani hawana kazi huku akihakikisha kwamba hata wavumilia wahandisi ambao hawajitumi na atawachukulia hatua lengo ni kuona kila mtendaji anawajibika.
Kwa upande wake Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pilli Mbaga amempongeza Waziri huyo wa maji kwa kazi nzuri anayoifanya kwani amekuwa wa mfano.
Amesema kuwa katika ziara ya kamati ya siasa iliyofanyika hivi karibuni ilibaini kuwa Wilaya ya Kondoa na Dodoma mjini eneo la nala ndio yenye changamoto ya maji .
Naye ,Mkurugenzi wa Mamalaka ya maji na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA Mhandisi Aron Kalambo akitoa tathimini ya mradi huo amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 96 na unaenda kutatua kero ya maji katika kata 10 jijini hapa.
Comments
Post a Comment