Na. Rhoda Simba, DODOMA
RAIS wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ametoa shilingi Bilion 1.3
kwaajili ya kumalizia mtambo wa usambazaji maji katika mradi wa Iyumbu.
Waziri Juma Aweso akisisitiza jambo
Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Waziri wa Maji, Juma Aweso
wakati akitembelea na kukagua mradi wa Maji wa Iyumbu na
Nyumba 300.
"Mradi huu ulikuwa unagharimu shilingi Bilion 2.7 na katika awamu ya kwanza Rais Samia ametoa Bilion 1.4 na fedha inayobaki itakamilishwa hivi karibuni" amesema Aweso.
Kadhalika kwa mamlaka aliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo aliyekuwa Meneja Ufundi Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dodoma mjini (DUWASA), Mayunga Kashilimu kuwa mkurugenzi huku Mhandisi James Ryoba aliyekuwa akijitolea kuagiza aajiliwe.
"Katika awamu ya kwanza Serikali iliahidi kuwa mradi huu ulipangwa kutekelezwa kwa kiwango cha Fedha cha bilioni2.7 na serikali kwa awamu ya kwanza ilitoa bilioni 1.4"amesema Aweso.
Aweso ametuma salamu kwa wahandisi wa Wizara hiyo kuhakikisha
wanafanya kazi kwa bidii kwa sababu wapo watalaam wengi wamemaliza vyuo na wapo mtaani hawana kazi huku
akihakikisha kwamba hata wavumilia wahandisi ambao hawajitumi na atawachukulia
hatua lengo ni kuona kila mtendaji anawajibika.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Dodoma, Pilli Mbaga amempongeza Waziri huyo wa Maji kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaja kuwa ni waziri wa mfano.
Aidha, amebainisha kuwa katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa iliyofanyika hivi karibuni ilibaini kuwa Wilaya ya Kondoa na Dodoma mjini eneo la Nala ndio yenye changamoto ya Maji.
Awali Mkurugenzi wa DUWASA, Mhandisi Aron Kalambo akitoa tathimini ya mradi huo amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 96 na unaenda kutatua kero ya maji katika kata 10 jijini hapa.
MWISHO
Comments
Post a Comment