Na. Noelina Kimolo, DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amesema kuwa UKIMWI bado upo hivyo serikali
imeweka malengo ya kuutokomeza ifikapo mwaka 2030.
Waziri Ummy Mwalimu |
Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua makasha ya
kusambaza kondomu pamoja na uzinduzi wa safari kondomu uliofanyika katika kituo
kikuu cha mabasi jijini Dodoma.
Waziri Mwalimu alisema kuwa ni muhimu kusambaza
kondomu katika halmashauri zote nchini ili ziweze kuwafikia wananchi na
kuendelea kuhamasisha wananchi kutumia kinga ili kuzuia ugonjwa huo.
“Si vibaya kwa msichana kuwa na kondomu kwa kuwa inaonesha
unajitambua, unajielewa na upo tayari kujikinga kwa sababu usipojikinga wewe
hakuna mtu mwingine wa kukukinga” alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma
Mganga alisema kuwa kondomu hizo zitasaidika katika kupunguza mimba za utotoni
haswa wanafunzi ambao wanasafari ndefu ya kutengeneza maisha yao.
“Kwa Mkoa wa Dodoma tunaadhirika sana na mimba za
utotoni kwa uzinduzi huu wa leo ninaamini tunakwenda kupunguza na kwa kufanya
hivi tunakwenda kupunguza pia watoto kutokumaliza shule” alisema Dkt. Mganga.
Wadau |
Dkt. Mganga alisema kuwa kwa kutumia kondomu
tunakwenda kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa kuwa ugonjwa huu umekuwa
ukigharimu serikali fedha nyingi kwa ajiri ya kununua ARV.
“Kwa zoezi hili la leo naamini tunakwenda kupunguza
mzigo wa ununuzi wa dawa hizo kwa sababu maambukizi yanakwenda kupungua na
fedha hizo zikatumika katika kuleta maendeleo ya Nchi yetu” alisema Dkt.
Mganga.
Nae Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof.
Davis Mwamfupe alisema kuwa kujikinga ni swala ambalo limesahaulika sana hivyo,
kutokana na uzinduzi huo utawasaidia watu wengi.
Prof. Davis Mwamfupe |
“Vijana niwakumbushe bado mnamuda mwingi wa kuishi
lakini msiwe katika vishawishi kwamba ikifika wakati mtafanya maamuzi sahiii
sio rahisi au ikifika mahari ntatumia kinga sio rahisi” alisema Prof. Mwamfupe.
Alisema kuwa waendelee katika kujikinga kwa muda wote
ili kujikinga na ugonjwa huo hivyo vijana wawe huru katika kutumika kinga hizo.
MWISHO
Comments
Post a Comment