Na. Revocatus Kassimba, RUKWA
Halmashauri
za mkoa wa Rukwa zimetakiwa kutumia fedha za serikali kuu na za makusanyo ya
ndani kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha huku
miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa shule, ujenzi wa hospitali na miradi ya maji ikiwa
na ubora.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (kulia aliyevaa kofia) akikagua eneo panapojengwa majengo ya wodi tatu za hospitali ya Mtowisa wilaya ya Sumbangwa |
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati alipofanya
ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga ikiwa na lengo la kufuatilia na kutilia mkazo utekelezaji wa kazi za
Serikali tangu alipoteuliwa kuongoza mkoa wa Rukwa hivi karibuni.
Mkuu
huyo wa Mkoa ameziagiza Halmashauri mkoani Rukwa kutumia fedha zake za
makusanyo ya ndani kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilishwa kwa ubora na
wakati ili kero za wananchi kukosa madarasa, maji na huduma za afya ikiwemo
ukosefu wa madawa.
“Sasa
Serikali imepunguza mzigo kwa halmashauri kwa kulipa posho za madiwani hivyo
tunategemea kuona fedha iliyokuwa ikilipwa kwao ikitumika kukamilisha miradi ya
maendeleo kwenye kata na vijiji “alisema Mkirikiti ambaye awali alikuwa Mkuu wa
Mkoa wa Manyara.
Mkirikiti
ambaye amembatana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba wakiwa
kwenye mradi wa ujenzi wa shule mpya ya kata kijiji cha Kalumbaleza walijionea
jinsi madarasa sita yakiwa yamekamilika kwa hatua ya renta kwa gharama ya
Milioni 11.5 ikiwa ni nguvu za wananchi mradi ulionza mwaka 2019.
Akiongeoa
kwenye mradi huo Mkuu wa Mkoa huyo wa Rukwa aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga kubadili utaratibu na kutumia mfumo wa kukamilisha ujenzi wa shule
moja kwa wakati badala ya kwenda na miradi yote.
“Halmashauri
wekeni kipaumbele kukamilisha ujenzi wa maboma ya shule zote tano kabla ya
Desemba mwaka huu kwa kuanza na shule moja
kila mwezi , hivyo Viongozi kazi
yenu ni kuhamasisha na kuwatambua wadau wakiwemo wananchi ili wachangie nguvu
na rasilimali fedha kukamililisha ujenzi huo” alisema Mkirikiti.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa kwenye Kitongoji cha Kipenzi Kijiji
cha Mfinga alikagua mradi wa maji uliogharimu fedha Shilingi Milioni 102 na
kubaini tatizo la uharibifu wa mazingira kwenye chanzo cha maji ambayo ni safu
za milima.
Mkuu
huyo wa Mkoa akiwa kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa maabara ya shule ya
sekondari Kikware Kata ya Mfinga iliyopo Bonde la Ziwa Rukwa alikemea kitendo
cha wataalam wa ujenzi wakiwemo wahandisi kuweka gharama kubwa za miradi kwa
kigezo cha makadirio ya kitaalam (BOQ) hali inayosababisha majengo ya Serikali
kutokamilika kwa wakati.
“Wananchi
wetu hawana dhambi tatizo ni wataalam wetu wa halmashauri maabara hizi
zinahitaji Milioni 30 lakini hadi sasa BOQ imewezesha maabara ya kemia pekee
bado ya Fizikia na Baiojia. BOQ ni tatizo. Wahandishi wa ujenzi fanyeni kazi
zenu kwa uhakika na ubora” alisema Mkirikiti.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti akishuka mlimani kutoka kukagua tenki la maji wakati alipotembelea mradi wa maji Kasekela kitongoji cha Kipenzi Kata ya Mfinga wilaya ya Sumbawanga |
Christina
Mpepo mkazi wa Kitongoji cha Kipenzi Kata ya Mfinga Sumbawanga alisema anaomba
Rais Samia Suluhu Hassan achukue hatua kali dhidi ya wanachi wanaoharibu
mazingira ikiwemo wanaochoma moto misitu.
Naye
Victoria Credo mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Milenia kata ya
Mtowisa aliwasilisha changamoto za ukosefu wa maji ,kutokuwepo kwa umeme na
tatizo la upungufu wa madarasa kuwa ni kikwazo kwa shule yao yenye wanafunzi
zaidi ya 530 kusoma vema.
Akizungumza
kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Apolinary Macheta alisema wamejipanga kukamilisha miradi ya
ujenzi wa shule nne za sekondari mwaka huu ili kuondoa upungufu wa madarasa pia
kuhakikisha miradi ya ujenzi ikiwemo hospitali ya Mtowisa majengo ya wodi tatu yanakamilika
kwa wakati.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti kesho anaendelea na ziara yake ya kukagua
miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi kwenye Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga.
Mwisho
Comments
Post a Comment