NEMC WASHIRIKIANA NA SUA KUZINDUA WARSHA YA MRADI WA UTAFITI WILAYANI MBARALI MKOANI MBEYA

Na. Mwandishi Wetu

 

Ni jukumu la kila mdau kama vile serikali za Mitaa, wakulima, wafugaji, jumuia za watumiaji maji, watunzaji wa mazingira na taasisi binafsi kuhakikisha kwamba rasilimali maji zote zinalindwa kikamilifu kwa ajili ya uendelevu wa madakio ya maji na maisha kwa ujumla.   

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Ruben Mfune, akifungua rasmi warsha ya uzinduzi wa mradi wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia Tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa Mazingira na utekelezaji wake katika kulinda ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na Athari za shughuli za Kubinadamu, Tanzania iliyofanyika Wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mh. Reuben Mfune ambaye alikua Mgeni Rasmi wakati wa warsha ya  uzinduzi wa Mradi wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzani(EFLOWS). Uzinduzi huo umefanyika Rujewa-Wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya.

Vilevile, Mheshimiwa Mfune, ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Mazingira (UNEP) kwa ufadhili wa kifedha katika mradi huo, pia Sekretarieti ya Azimio la Nairobi (Nairobi Convection Secretariat) ambayo ni msimamizi wa utekelezaji. Pamoja na Waratibu wa mradi huo kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kujitoa kwao kutekeleza mradi huu ambao ni mojawapo ya miradi iliyopo katika nchi zilizo kwenye Mpango Mkakati wa nchi za Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi 

 

Sehemu ya washiriki wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia Tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa Mazingira na utekelezaji wake katika kulinda ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na Athari za shughuli za Kubinadamu, Tanzania wakisikilia maelezo yanayotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Ruben Mfune (hayupo pichani).

Aidha, amesema kuwa anafurahi  kuona kwamba masuala ya mazingira kama vile umwagiliaji, kilimo kandokando ya kingo za mito, ufugaji wa mifugo ndani ya kidakio cha mto Mbarali na Bonde la Rufiji pamoja na ongezeko la watu, vinasimamiwa kwa uhifadhi kamilifu wa eneo la Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi. Na muhimu zaidi kwa ajili ya mtiririko endelevu wa maji kuelekea Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project - JNHPP).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC katika hotuba yake ya ukaribisho kwa mgeni Rasmi iliyosomwa kwa niaba yake na Meneja wa Utafiti-NEMC Bi Rose Salema Mtui amesema kuwa NEMC kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma/utafiti zimekuwa zikitengeneza miradi/programu  na kufanya tafiti na mojawapo ni kama mradi huo uliozinduliwa kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali ya kimazingira. 

“Kupitia mradi huu, utekelezaji wa mtiririko wa maji kwa mazingira (env. flow) ni muhimu sana kwa uendelevu wa ikolojia ya mto; na natumaini wadau wote na Serikali kwa ujumla watakuwa tayari kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha malengo ya mradi huu yametimia” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Ruben Mfune akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia Tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa Mazingira na utekelezaji wake katika kulinda ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na Athari za shughuli za Kubinadamu, Tanzania


Akiongea katika warsha hiyo ya Uzinduzi Mkurugenzi wa Shahada za Juu Uhawilishwaji wa teknolojia za Kitafiti kutoka Chuo Cha Sokoine SUA Profesa Ezron Karimuribo  amesema kuwa kuna uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji Nchini na umetokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama vile ukataji miti, uchomaji misitu, kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji, uchimbaji madini,ufuagji na uchepushaji wa maji. Hivyo basi katika mradi huo ambao utafanyika katika wilaya ya Mbarali  na wilaya hiyo imechukuliwa kama kianzio tu.

Mradi huo utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzani (EFLOWS unaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.