Na. Mwandishi Wetu, NYASA
Naibu waziri wa Wizara ya maliasili na Utalii, Mary
Masanja (Mb), Amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa, kutangaza Utalii wa Fukwe
na Vivutio vingine Vya asili vilivyoko katika Wilaya ya Nyasa,ili wawekezaji
wavifahamu na waje kuwekeza kwa kuwa ni
vivutio vizuri na havipatikani sehemu nyingine.
![]() |
Naibu waziri wa Wizara ya maliasili na Utalii, Mary Masanja |
Ameyasema hayo leo alipotembelea na kufungua
Bustani ya mawe iliyopo katika Kata ya Kihagara Wilayani Nyasa, kwa lengo la
Kutangaza Utalii wa FUKWE za Ziwa Nyasa ambazo ni za asili na ni nzuri
zinazoweza kuwavutia Wawekezaji kama zitatangazwa.
Masanja amefafanua kuwa, ametembelea katika Bustani
ya Mawe ameona na amevutiwa na Vivutio vilivyopo katika eneo la Bustani hiyo na
kuvitaja baadhi ya Vivutio hivyo kwa ni pamoja na Mamba anayeitwa na kutii,
Bustani nzuri ya mawe yaliyojipanga vizuri, lakini ndani yam awe hayo kuna
sehenu nzuri ya kukaa na mke mliyegombana na mkitoka hapo upendo unaanza upya
na unazidi.
Ameongeza kuwa kivutio kingine ni Ngoma za asili
ambazo huwezi kuziona Sehemu nyingine isipokuwa Nyasa, ngoma hizo ni Mganda,
kioda ambacho wanacheza kwa Stali mbalimba ambazo zinamvutia Mtalii yeyote
atakayefika katika eneo hilo
Leo niko hapa katika Bustani ya Mawe iliyopo kata
ya Kihagara katika Fukwe za Ziwa Nyasa, ni Nzuri na zinafaa kwa Utalii wa
Ndani,wito wangu kwenu wananyasa ni kuitangaza Wilaya ya Nyasa ili wawekezaji
waweze kuja kuwekeza Wilaya ya Nyasa, kwa kuwa leo nimeona Mamba unayemuita
akaja kula chakula, Fukwe Nzuri za Ziwa Nyasa, Lakini nimepanda kwenye boti na
kujionea fahari ya Ziwa Nyasa. Mimi ninaanza kuitangaza Wilaya ya Nyasa na sisi
wenyewe titangaze Wilaya ya Nyasa.
Ametoa wito kwa Wawekezaji kuja kuwekeza Wilaya ya
Nyasa kwa kuwa ni wilaya iliyosheheni fursa mbalimbali za utalii na kila kitu
kinapatikana Nyasa.
MWISHO
Comments
Post a Comment