Na. Netho C. Sichali, NYASA
Mbunge
wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, amemshukuru na Kumpongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa Kutekeleleza
Miradi ya Maji Wilaya ya Nyasa.
Ameyasema
hayo jana alipotembelea na kukagua miradi ya maji ya Ukuli, Kingerikiti na
Mradi wa Kijiji cha Lundo, Kata ya Lipingo, Miradi ambayo imetatua kero ya
wananchi wa kata ya Kingerikiti na Lipingo Wilayani Nyasa.
Mhandisi
Manyanya amefafanua kuwa, Ukuli kingerikiti na Mradi wa maji wa Kijiji cha
Lundo kata ya Lipingo ni Miradi ya maji ambayo ilikuwa ikimnyima usingizi kwa
kuona wananchi walivyokuwa wakiteseka kuchota maji umbali mrefu lakini leo
amefurahi kuona kero ya maji imekwisha, wananchi wakipata maji bombani.
Manyanya
ameongeza kuwa anamshukuru kwa dhati, Mh. Rais kwa sababu Serikali imempa fedha
ya kutatua Kero ya maji ya katika kata hizo na Miradi mingine ikiwa inaendelea
kutekelezwa, katika kijiji cha Likwilu na Ngingama ili kuendelea kutatua Kero
ya Maji wilayani Nyasa.
Aidha,
amesema Wilaya ya Nyasa bado ina changamoto ya Upatikanaji wa maji safi na
salama katika maeneo mengine hivyo bado anaomba asaidiwe miradi mingine ya maji
katika Kata zilizobaki.
Aidha,
ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuitunza miundombinu ya maji
iliyotengenezwa na Serikali na kuunga juhudi za Serikali kwa kuchangia gharama
ndogo za ukarabati.
Comments
Post a Comment