Na. Netho C. Sichali, NYASA
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya
ya Nyasa, Jana imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo 4 wilayani
Hapa na kuridhishwa na maendeleo ya Miradi hiyo.
Miradi Iliyotembelewa ni Ujenzi wa Ujenzi wa
Matundu Saba ya Vyoo na kuona jinsi huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi,
katika Kituo cha Afya Mbamba Bay, Mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya
ya Nyasa, Mradi wa Maji Ukuli Kingerikiti, na Mradi wa Maji wa Kijiji cha Lundo
Kata ya Lipingo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyasa Krodvic Duwe
ambaye ni Mkuu wa Msafara wa Ziara hiyo amesema lengo la Ziara hiyo ni wajumbe
waweze kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo ambayo inalenga kutatua changamoto
za wananchi kwenye sekta za afya, Maji na Utawala.
Duwe katika Majumuisho ya Ziara hiyo, amesema
kamati ya Siasa Wilaya ya Nyasa Imeridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Miradi
ya Maendeleo, na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Kanali Laban
Thomas, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Bw. Jimson Mhagama na Mbunge wa
Jimbo la Nyasa kwa Kutekeleza Miradi hiyo kwa Ufanisi.
Akiwa katika Kituo cha afya Mbamba bay, alikagua
ujenzi wa Vyoo wenye lengo la kutatua changamoto ya Upungufu wa Vyoo na
kuridhishwa na hatua ya Utekeleza wake na kamati ilipata fursa ya kuongea na baadhi
ya weagonjwa na wananchi, waliokuwepo maeneo ya Kituo cha afya na wakasema
wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na watumishi wa Afya, Kituo cha Afya cha
Mbamba Bay, na kuupongeza uongozi wa Wilaya kwa kuboresha na kutoa Huduma Bora
kwa Wananchi.
Katika Mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
ya Nyasa, Kamati Pia Imeridhishwa na Ujenzi huo ambao umefikia hatua ya
kukamilika kwa boma na Kumtaka Mh. Mbunge wa Jimbo la Nyasa kufuatilia kwa
uKaribu Fedha za kumalizia Ujenzi.
Katika Miradi ya Maji ya Ukuli Kingerikiti kamati
imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na
Wizara ya Maji kwa kutatua changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wananchi wa
Ukuli Kingerikiti, kwa kutoa fedha za ujenzi na Ukarabati wa Mradi huo na kwa
sasa wananchi hawana kero ya maji na wanafurahia huduma hiyo.
Katika Mradi wa Maji wa Kijiji cha lundo Kata ya
Lipingo kamati imejionea kwa Dhati Serikali ilivyotatua kero ya maji katika
Kata ya Lipingo mradi ambao utamaliza kero ya maji Katika Kata hiyo na imemtaka
meneja wa RUWASA Mhandisi Evaristo Ngole, kusambasa maji hayo katika kata ya
Lipingo na Liuli kwa kuwa maji ni Mengi yatakayokidhi walaji wa Kata ya Lipingo
na ziada kubaki.
Ziara hiyo Imeambatana na Viongozi Wafufatao Mbunge
wa Jimbo La Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, kanali Laban
Thomas na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama.
Comments
Post a Comment