FANYENI AJENDA YA UPATIKAJI WA DAWA IWE YA KUDUMU: DKT. GWAJIMA

Na. WAMJW- Dodoma.

 

Wafamasia nchini wametakiwa kufanya ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kudumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa.

 

Dkt. Gwajima pia akizindua Mwongozo wa Usimamizi wa Maduka ya Dawa yanayoendeshwa na vituo vya kutolea huduma za afya vya Umma.

Rai hiyo imetolewa leo na Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa bidhaa za afya kwa wafamasia wa Mikoa, Halmashauri na Hospitali uliofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema kuwa ajenda hiyo ikiwa endelevu Kwenye ngazi hizo Basi hakutakuwa na malalamiko ya upatikanaji wa dawa yanayoendelea kuwa hauridhishi 

"Nitoe maagizo kwa viongozi wa ngazi zote, wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali fanyeni ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kidumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa".Alisisitiza.

Hata hivyo Dkt. Gwajima aliwataka wafamasia hao kuimarisha kamati za Dawa na Tiba Katika ngazi zote "Mfamasia  ndiye Katibu wa kamati za Dawa na Tiba lakini kamati hizi hazifanyi kazi zimekufa, naelekeza kuwa wote ambao kamati zao zilibainika kuwa mfu watoe maelezo kwa mamlaka zao za ajira na kwa Baraza lao la kitaaluma.

Aidha, Waziri huyo aliwaagiza wataalamu hao kwenda kusimamia Mwongozo wa Matibabu nchini na Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (STG/NEMLIT), kwani mwongozo huo toleo jipya la mwaka 2021 limezinduliwa.

Wafamasia wanaoshiriki mafunzo hayo wakifuatilia Waziri wa Afya Dkt. Gwajima (hayupo pichani) Kwenye ufunguzi huo jijini Dodoma


"Andikeni dawa kwa kuzingatia mwongozo huu na kuwe na mfumo wa tathmini kwa wale wasiotii kuandika majina halisi ya dawa (generic names) Bali wanaandika majina ya Biashara zao (brand names) mkasimamie mwongozo huu"Alisema.

Kwa upande wa matumizi ya Cheti Cha Dawa Dkt. Gwajima aliwataka wafamasia hao Kwenye kusimamia Hilo Kama alivyoelekeza awali kanuni ya cheti cha dawa 'The Pharmacy (Prescription Handling and Control Regulations, 2020) kwani imeandaliwa na imeanza kutumika.

"Sekta ya afya na hasa waandishi na watoaji wa dawa fuatieni kanuni hii kinyume na hapo utashtakiwa tu maana haitajulikana Nani alikunywa dawa".

Dkt. Gwajima aliwataka wafamasia hao kuhakikisha Kuna upatikanaji na matumizi sahihi ya nyezo muhimu za usimamizi wa bidhaa za afya zikiwemo leja ya mali na hati yabkutoa na kupokea mali, rejista ya dawa, rejista ya sindano na cheti cha dawa.

 

Mwisho

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.