WAZEE wa Mkoa wa Ruvuma wamefanya
kikao maalum cha uundaji Baraza la Wazee la Mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi
wa mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.
Waliochaguliwa kuunda Baraza hilo
kwenye uchaguzi ulishirikisha wawakilishi kutoka wilaya za Nyasa,Mbinga,Songea,Tunduru
na Namtumbo ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa amechaguliwa Elenzian Nyoni kutoka Manispaa ya Songea.
Wengine waliochaguliwa ni Lusiana
Nduguru kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambaye amechaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti,Katibu ni Winfrid Mbilinyi kutoka Halmashauri ya Madaba na Naibu
Katibu Philipo Katyale kutoka
Halmashauri ya Songea.
Viongozi wengine waliochaguliwa kuunda
Baraza la Wazee wa Mkoa ni Mtunza Hazina amechaguliwa Esta Nzuyu kutoka
Halmashauri ya Mji wa Mbinga,Mwakilishi wa wanaume Yustin Mande kutoka
Halmashauri ya Nyasa na Mwakilishi wa wanawake amechaguliwa Maria Luoga kutoka
Manispaa ya Songea.
Akizungumza wakati anafungua kikao cha
uchaguzi huo,mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bakari Ally
Mketo amesema Taifa linawategemea sana wazee ambao ni hazina kubwa katika
jamii.
“Taifa bila wazee halina dira,wala
muelekeo,sehemu yeyote panapokosekana wazee,pana hatari ya kuangamia’’,alisisitiza
Mketo.
Amesema vijana wana mengi ya kujifunza
kutoka kwa wazee kwa sababu wazee wanafahamu siri kubwa na hekima ya kuwa kiongozi bora ambapo
amesisitiza kuwa Taifa linawategemea wazee ndiyo maana yanaundwa mabaraza ya
wazee katika ngazi mbalimbali.
Amesema serikali imetoa nguvu kubwa
katika mabaraza ya wazee na kwamba
busara ya wazee kwenye mabaraza hayo
itasaidia kutafutia ufumbuzi changamoto
mbalimbali zinazowakabili wazee.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Juni 29,2021
Comments
Post a Comment