Na. Mwandishi
Wetu, DAR ES SALAAM
Wataalam
kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara, wameanza kutoa
elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa
ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
|
Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kuanza kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Katika
Maonesho hayo wananchi wanaelezwa kuhusu masuala mbalimbali kama utekelezaji
miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme pamoja na
Gesi Asilia.
Aidha,
Wataalam hao wanapokea maoni na kutoa huduma mbalimbali ya wananchi na kuyafanyia
kazi kwa kushirikiana na Taasisi zilizo chini ya Wizara zinazoshiriki Maonesho
hayo.
Taasisi
zilizo chini ya Wizara zinazoshiriki Maonesho hayo ni pamoja na Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa
Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).
|
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Shukrani
Rugaimukamu akitoa elimu mwananchi aliyefika katika Banda la Nishati
katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Kauli Mbiu ya
Maonesho hayo ni, Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu ambapo
nishati ni injini ya kuwezesha uchumi huo wa viwanda.
|
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati (kutoka kushoto), Jacob Mayalla, Shukrani Rugaimukamu na Mussa Abbas wakimsikiliza mwananchi aliyefika katika Banda la Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
|
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mussa Abbas akitoa elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
|
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Jacob Mayalla (katikati) akitoa elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Comments
Post a Comment