Na Rhoda Simba Dodoma.
KATIKA kuendelea kukuza na kutangaza utalii wa ndani hapa nchini, Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA limetoa mafunzo ya uhamasishaji utalii wa ndani kwa wadau wa utalii Kanda ya Kati na kusini mwa Mikoa ya Iringa na Mbeya lengo likiwa ni mpaka kufikia 2025 wafikie watalii 5000 hadi 6000 .
Akifungua mafunzo hayo Jijini Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi,Ahmed Mbugi amesema licha ya changamoto ya ugonjwa wa covid 19 (Corona )hawana budi kuona ni njia gani zitazosaidia kuongeza utalii wa ndani haswa kwa wazawa.
Amesema kupitia mafunzo hayo ni kuhakikisha wadau wa utalii kuona ni mbinu gani zinaweza kutumika ili wazawa na wadau wengine wapende utalii hasa wa ndani badala ya kusubiri wageni kutoka nje.
"Wote kwa pamoja tunawajibu wa kutekeleza utalii wa ndani kwani unamlenga kila mtanzania kuanzia ngazi ya Chini,Kati mpaka kiwango Cha juu "amesema Mbugi
Aidha akitoa maelezo juu ya wananchi kuogopa kwenda hifadhini kutokana na gharama amesema kuwa Shirika la TANAPA limeweka bei tofauti ambayo ni rahisi na kumudu kwa kila mtanzania tofauti na mtalii kutoka nje ya nchi.
"Tukiendelea kuweka gharama za juu za kutalii sisi Kama Shirika tutapata hasara Mara mbili na hata kwenye uwekezaji tutapata hasara bila kusahau hata nyinyi wadau kwa mmoja mmoja mtashindwa kujipatia kipato"Amesema Kamishina Mbugi
Amesema umuhimu wa utalii wa ndani Ni pamoja na kutembelea vivutio vya ndani ili wananchi waweze kuchangia Pato la Taifa.
"Tunapozungumzia utalii wa ndani ni pamoja na kujifunza jiographia halisi ya sehemu husika kupumzisha akili na kujifunza vitu vingine mbalimbali"amesema Mbugi
Wakiongea kwa nyakati tofauti wadau hao wa utalii wamesema changamoto ni kwamba elimu bado haijawafikia wadau husika wa utalii ambapo wameomba elimu ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili watoto wanapokua wajue kwamba utalii ni utamaduni wao.
Naye Irene Kitambi kutoka Utulivu Tours for Rravel Iringa amesema changamoto wanazokutana nazo ni miundo mbinu mibovu ya barabara inayowafanya watalii kuogopa kwenda kutalii kipindi Cha msimu wa Mvua.
Mwisho
Comments
Post a Comment