SERIKALI YATOA WITO KWA NYUMBA ZA IBADA,KUMBI ZA STAREHE ,BURUDANI KUHUSU UCHAFUZI WA MAZINGIRA UTOKANAO NA KELELE NA MITETEMO
Na Jackline Kuwanda,Dodoma
Serikali imetoa wito kwa wamiliki wa Nyumba za
Ibada,kumbi za Starehe na Burudani kuhakikisha sauti zinatokanazo na shughuli
zao hazizidi viwango vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria.
Pia imetoa wito kwa wamiliki wa maeneo ya Burudani
na Starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia suati kama
ilivyoelekezwa kwenye masharti yote ya leseni zao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini
Dodoma Waziri nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Suleiman
Jafo amesema hiyo ni kufuatia kuongezeka
kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele na mitetemo hali
iliyosababisha utoaji wa taarifa za malalamiko juu ya hali hiyo.
‘’katika kipindi cha mwaka 2019/2020 NEMC
ilipokea jumla ya malalamiko 165 kutoka Mikoa ya Dar es salaam ,Dodoma ,Arusha ,Mbeya ,Mwanza ,Morogoro
na Tabora ambayo yalihusisha kelele kutoka kwenye nyumba za ibada,kumbi za
starehe na baa na maeneo yanayoongoza kulalamikiwa ni maeneo ya nyumba za
starehe na burudani na nyumba za Ibada’’amesema Jafo
Waziri Jafo ameendelea kutoa wito kwa yeyote
atakaye sababisha kero zinatokanazo na kelele za mitetemo kinyume na kanuni ya
usimamizi wa Mazingira za mwaka 2015 kuwa adhabu yake itakuwa ni faini
isiyopungua shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi sita.
‘’Adhabu hiyo itaendana na na kufungiwa kwa
biashara husika,wananchi pia mhakikishe agenda ya kelele na mitetemo inakuwepo
kwenye mikutano ya makazi,mnaombwa pia kutoa taarifa kuhusu kero 3 ya kelele ya
mitetemo kwa Ofisi za Serikali za Mitaa au NEMC kwa namba za bure
(1800110115,0800110117 na 0800110116) amesema Jafo
Waziri jafo amefafanua kuwa lengo kuu la
kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa kelele na mitetemo) za mwaka 2015
pamoja na mambo mengine ni kulinda afya ya binadamu na mazingira kutokana na
matatizo mbalimbali kama vile kupoteza usikuvu.
‘’kuondosha utulivu,kupunga ufanisi wa
kazi,kuzuia watu wasipate usingizi,athari za kisaikolojia kwa watoto,magonjwa
ya moyo,usumbufu kwa wagonjwa,kupunguza umajini wakati wa kujisomea na kero kwa
jamii’amesema Jafo
Kwa upande wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema watu wataendelea kuelimishwa ili kuachana na kadhia hizo ambazo zimekuwa zikisababisha athari kwa watu
‘’tutaendelea kuelimisha watu waeleewe na waone na waache kusababisha madhara kwa
wengine na watakao shindwa kufanya hivyo sisi wenyewe tutawaripoti sababu
wanatuongezea wagonjwa wadini unakuta na wengine uwezo wa kujitibia hawana mpaka
serikali inawatibu kwa msamaha ‘’amesema Dkt Gwajima
Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira , Ofisiya Rais TAMISEMI,Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto,Wizara ya Viwanda na Biashara ,Wizara ya Elimu ,Sayansi
na Tekinilojia na Wizara ya Mambo ya ndani zimeungana kwa pamoja kuhakikisha
kuwa Afya ya jamii inalindwa kutokana na athari zitokazo na kelele na mitetemo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment