Na. Pendo Mangala, DODOMA
SERIKALI imesema kuwa nchi ina ulazima wa kuwa na
mpango wa kitaifa wa kupambana na umwagikaji mafuta Baharini na Maziwa makuu
pale inapotokea ajali za meli za usafiri wa abiria na mizigo kwani
umwagikaji wa mafuta hayo unaathiri uchumi wa nchi na kuua vimbe ambavyo
vinaishi Baharini.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Wa Usalama na
Mazingira wa Wizara Ya Ujenzi Na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi,Bi.Stellah Katond
kwenye kikao cha Shirika la uwakala wa Meli Tanzania TASAC, na wadau mbalimbali
kinacho jadili mpango wa kitaifa wa kupambana na umwagikaji mafuta
Baharini na Maziwa Makuu ambapo amesisitiza kuwepo kwa Mpango wa kusafisha
mafuta baharini kwa haraka inapotokea Dharura.
Mkurugenzi Katondo, amesema lengo la Mpango huo wa kitaifa ni kusadia kupambana na umwagikaji wa mafuta bahari pamoja na maziwa makuu.
Amesema kuwa mpango huo ulikuwepo toka mwaka 2016, lakini hivi
sasa umehuwishwa kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza katika sekta
hiyo.
“Awali mpango huu ulikuwa chini ya Sumatra lakini kutoka na
Sumatra kuvunjwa serikali iliamua kuuleta katika shirika la Uwakala wa meli
(Tasac) ili kuweza kuutekeleza kwa kushirikiana na wadau wengine”alisema
Katondo.
Pamoja na mambo mengine amesema Tanzania ni moja kati ya nchi
zinazohusika katika usafirishaji baharini na kwenye maziwa makuu na vyombo
hivyo vinatumia mafuta na vinabeba mizigo ya nishati hiyo mpango huo utasaidia
kuwepo na namna nzuri ya kusafisha pale yanapofuja.
Kwa upande wake Kaimu Msajili Wa Meli ALFREDI WARIANA akaeleza mpango huo namna utakavyosaidia kupangilia vifaa na nyenzo ambazo zinatakiwa kutumika pale madhara yanapojitokeza ya umwagikaji wa mafuta baharini wakati nchi ya Tanzania na Uganda zinatarajia kujenga mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima uganda kwenda Chongoleani Tanga.
“Lakini mpango huu utawezesha kusadia kupata msaada kwa mataifa
mengine yenye vifaa vya kisasa pale linapotokea janga kubwa la kuvunja kwa
mafuta baharini ili kusaidia kuyaondoa kabla ya kuleta athari kubwa kwa viumbe,
pia mpango huu utasaidia kujenga ushirikiano na mataifa mengine”alisema
Naye Mhifadhi, ufundi na uwezeshaji wa hifadhi za bahari nchini
Clever Mwaikambo, amesema wanaishukuru serikali kwa kufanikisha kupatikana kwa
mapango huo ambao utakuwa mkombozi wa mazingira na kulinda uchumi wa bluu.
Amesema kuwa ni lazima taifa kuwa na vifaa vya kusafisha na
kuondoa mafuta pale yanapovuja baharini ili mazingira kuendelea kubaki salama
pamoja na viumbe vilivyomo.
MWISHO
Comments
Post a Comment