NEC YA CCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI KAZI

Na. Rhoda Simba, Dodoma

 

HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM  ya Taifa (NEC) imekutana leo jijini Dodoma katika kikao cha kwanza na kumpongeza  Rais Samia Suluh Hassan kwa kuivusha nchi  salama katika  kipindi cha mpito baada ya kuondokewa na aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli huku Taifa likibaki kuwa na amani na utulivu.

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka

Akizungumza leo na waandishi wa habari Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka amesema  kikao hicho kimeazimia pongezi hizo wampe kwa maandishi kwa kumpongeza kwa  kupokea madaraka katika kipindi kigumu.

"Wajumbe  wa Halmashauri kuu wameona anaenda vizuri katika uongozi wake kwa kuongoza kwa uadilifu na haki kwa kusimamia misingi ya kidemokrasia" amesema Shaka.

Aidha, amesema katika azimio lingine la kikao hicho wajumbe wameona Serikali yake imeendelea kuwajali wananchi wa chini hasa katika bajeti iliyowasilishwa ya 2021/22 kwani imetoa dira inayoonesha   serikali inakwenda kupambana na umasikini kwa vitendo.

Katika hatua nyingine Halmashauri kuu imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hussein Ally Mwinyi kwa kusimamia vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM)huko Visiwani Zanzibar 

"Kwa upande wa kiuchumi wa blue umeonekana wawekezaji wameendelea kujitokeza huku Amani na utulivu ikizidi kuimarika"amesema Shaka

Shaka amesema Rais Samia Katika kikao hicho amewasisitiza wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa kwamba bado wanajukumu kubwa la kwenda kusimamia Ilani huku akiwataka kusimamia miradi yote ambayo inatekelezwa na Serikali ili imalizike haraka na kwa wakati.

Pia amewataka kupokea Maelekezo na wasiwe na uoga Wala hofu bila kusita kusema Kama miradi hiyo haitekelezwi ipasavyo hivyo kuhakikisha miradi iliyoanzishwa itatekelezwa kwa wakati na ufanisi.

Kikao hicho Cha Nec kilikuwa Ni kikao Cha kawaida kwa mujibu wa katiba ya Chama  ambacho ufanyika kila baada ya miezi sita.

 

Mwisho.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.