MBEGU ZATOLEWA KWA WAKULIMA KUENDELEZA KILIMO KWA WAKULIMA

 



Na Muhammed Khamis

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ugawaji wa mbegu mbali mbali kwa wakulima wa mradi wa VIUNGO umezinduliwa leo kwa upande wa Unguja ambapo wakulima kutoka kanda ya Magharib na Kaskazini Unguja wamegawiwa mbegu tofauti zikiwemo za vanila mboga mboga pamoja na matunda.

Azungumza katika ugawaji wa mbegu hizo meneja utekelezaji wa mradi wa VIUNGO  kanda ya Unguja Bi Khadija Ali Juma alisema mbegu hizo zimetolewa kwa lengo la kuendeleza kilimo kwa wakulima hao ambao walipatiwa  mafunzo maalumu ya kilimo bora kupitia mradi huo.

Juma ya wakulima 238 wamepatiwa mbegu hizo kwa hatua ya awali ambao ni miongoni mwa wakulimua waliokwisha taarisha mashamba yao kwa ajili ya kuanza kushughuli za kilimo ikiwemo kupanda mbegu.

Aidha Bi Khadija aliwataka wanufaika  wengine wa mradi huo kuwa tayari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanataarisha mashamba yao ili waweze kuwa miongoni mwa wanufaika wa hatua za mwanzoni.

Akifafanua zaidi kuhusu ugawaji wa mgebu hizo kwa upande wa vanila alisema jumla ya miche 2700 imetolewa na kugawiwa kwa wakulima 27 ambapo kila mmoja atapata miche 100 ya vanila kwa ajili ya kupanda kwenye shamba lake mwenyewe baada ya kupatiwa elimu kupitia shamba darasa lililoanzishwa katika shehia hiyo.

Katika hatua nyengine meneja huyo alisema kwa upande wa bustani za nyumbani( kitchen garden) hadi sasa wakulima 80 wamejitokeza na wapo tayari kuanza kilimo hicho na ametoa wito kwa wanawake wengine kujitokeza kwa wingi ili waweze kujifunza mbinu bora za kilimo hicho zitakazo wasadia kupata lisha bora na kipato.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mkulima wa vanila kutoka kizimbani Unguja Haji Abdalla Abeid alishukuru mradi wa VIUNGO  na alisema utolewaji wa mbegu hizo kwao ni jambo muhimu na linalopaswa kupongezwa.

Alisema kwa muda mrefu wamekua wakipata wakati mgumu wanapohitaji mbegu za vanila kutokana na gharama yake, lakini kupitia utekelezaji wa mradi wa VIUNGO wameweza kupatiwa mbegu hizo bure bila ya gharama yoyote jambo ambalo limeongeza ari katika kuendeleza kilimo hicho.

Madi wa viungo ni wa miaka minne ambao unatekelezwa na asasi tatu za kirai ambazo ni PDF,CFP,TAMWA-ZNZ na unatarajia kuwafikia wanufaika 57,974 katika shehia 60 za Unguja na Pemba na umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya(EU).

Mwisho.

 

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.