Na WAMJW-ARUSHA
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, ambaye amemwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali Bi. Vones Oisso
amewaagiza Wamiliki wa Maabara binafsi za afya na Wataalamu wa Maabara
kusimamia utoaji huduma bora kwa kwa kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa
na Wizara ya Afya ili kupunguza matumizi holela ya dawa yanayoweza kuathiri
afya ya mgonjwa.
Bi. Oisso ameyasema hayo
leo katika kikao na Wamiliki Wa Maabara Binafsi za afya Mkoani Arusha, chenye
lengo la kuwashirikisha wamiliki wa Maabara Binafsi za Afya Mkoa wa Arusha ili
kupata uelewa wa pamoja kuhusiana na Sheria, Kanuni na taratibu zinazoelekeza.
“Nichukue nafasi hii
kuwaomba msimamie vizuri Maabara zenu ili kutoa huduma zenye ubora
kutokana na viwango ili kupunguza matumizi mabaya ya dawa, muda wa kutafuta
huduma pamoja na gharama za matibu kama watapata huduma kwa wakati” Amesema
Bi.Oisso.
Kwa upande mwingine
ameagiza maabara binafsi zote zihakikishe zinalipa ada kila mwaka bila
kuchelewa kwani kutofanya hivyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Maabara
binafsi nchini na hatua kali zitaanza kuchukuliwa kwa watakaokiuka utaratibu
huo.
“Ninajua kuwa kwenye
Mikoa yenu kuna Maabara nyingi za binafsi ambazo zimesajiliwa na zinalipia ada
kila mwaka na nyingine hazilipi ada za mwaka, hivyo hakikisheni Maabara zote
zinalipa ada ya mwaka, na zile zisizosajiliwa (Bubu) hakikisheni zinasajiliwa”
amesema.
Aidha, ameweka wazi
kuwa, zipo changamoto nyingi zinazosababishwa na Wamiliki wa maabara binafsi,
zikiwemo Kuajiri watu wasio na utaalamu pamoja na usajili kutoka kwenye Baraza
la Watalaam wa Maabara, Kutosajili Maabara zao na wale waliosajili hawalipi ada
ya kila mwaka, Kuanzisha Maabara sehemu ambazo hazitakiwi kuwa na Maabara.
Aliendelea kusema kuwa,
changamoto nyingine ni kama, Kuwa na jengo ambalo halikidhi viwango vya ubora
wa maabara, maabara kutofuata misingi ya ubora (Quality Management
System), mashine za maabara kutofanyiwa matengenezo kinga (PPM) na maduka ya
dawa kufanya vipimo vya maabara.
Comments
Post a Comment