WANAWAKE NA WASICHANA KUKOSA MAZINGIRA RAFIKI WAKATI WA HEDHI


 


Na Jackline Kuwanda, Dodoma.

Imeelezwa kuwa wasichana na wanawake katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto na mazingira yasiyo rafiki wakati wa hedhi hususani upatikanaji wa maji safi na salama.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto anayeshughulikia Maendeleo ya jamii Mwanaidi Ali Khamis katika maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani yanayoadhimishwa May 28 ya kila mwaka yaliyobeba kauli mbiu isemayo ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhakikisha vifaa vya kujisitiri/taulo za hedhi zinapatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa msichana/mwanamke.

‘’kwa mujibu wa shirika la watoto Duniani UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO  ya mwaka 2013 linabainisha kuwa katika kila msichana mmoja kusini mwa jangwa la sahara anakosa kwenda shule sababu ya kuwa kwenye hedhi ,asilimia 52 ya vyoo vya wasichana  havina milango na asilimia moja ya shule zimejenga shule kwaajili ya wasichana  kujisiriti wakiwa kwenye hedhi’’amesema Mwanaidi

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ahmad Makuwani amesema lengo la kukutana katika maadhimisho hayo ni Kujadiliana na kuvunja ukimya kwa kupaza sauti kwa jamii  kuhusiana na umuhimu wa hedhi salama kwani suala la hedhi limekuwa likichukuliwa kwa usiri kutokana na mila na tamaduni zilizopo.

‘’Lakini pia kuonesha umuhimu wa usimamizi mzuri wa wasichana katika suala la hedhi salama,kulingana na mila zetu suala la hedhi limekuwa likichukuliwa kwa usiri mkubwa sana hivyo kupitia maadhimisho haya yanasaidia kupaza sauti na kuvunja ukimya kuachana na dhana hiyo ‘’amesema 

Akitoa salamu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa TAMISEMI Fatuma Nasoro amesema ni wakati wa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa kuna kuwa na hedhi salama kwa wanawake na watoto wa kike huku akiwapongeza wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu na kusaidia vifaa mbalimbali ambavyo huwasaidia wanawake na watoto.

‘’Elimu hii itawafikia wadau wengine ambao hawako hapa nawapa moyo wadau wote tuko pamoja nanyi katika masuala haya yote yanayohusu hedhi salama’’amesema Fatuma

Mwenyekiti wa Jukwaa la Hedhi Salama kutoka Wizara ya Afya  Salavata Silayo amesema lengo la jukwaa hilo ni kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana wakati wa hedhi na kuwawezesha kuwa na uelewa juu ya hedhi salama.

’Jukwaa hili lilianza May 2020-2021 na kazi zinatekelezwa na Wizara pamoja na jukwaa la hedhi salama,jukwaa linampango mkakati wa miaka mitano wenye lengo la kuhakikihsa wanawake na watoto wanakuwa na hedhi salama’’amesema

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu amesema kutokana na jitihada za wadau katika kusaidia wasichana na wanawake zimesaidia watoto wa kike kusoma katika mazingira mazuri bila ya kuwa na changamoto yeyote ile.

Katika kuadhimisha siku hii wadau mbalimbali jijini Dodoma Dodoma News Blog imezungumza na wakazi mbalimbali jijini Dodoma akiwemo Babu Ally amesema  amesema kwa upande wa wanaume ni ngumu kulizungumzia kutokana na tamaduni zilizojengeka kuwa suala hilo linamuhusu mama pekee na si baba .

"Nafikiri Elimu juu ya umuhimu wa hedhi salama iendelee kutolewa kwa jamii hasa vijiji wengi hawana uelewa lakini kwa upande wa wanaume bado ni Changamoto kulizungumzia "kulingana na  tamaduni zetu nadhani watoto waongee na mama zao ila kwa wanaume inakuwa ni ngumu " Babu Ally 

Mama Simba  amesema kwa zamani wazazi walikuwa wakipeana majukumu pindi mtoto anapoingia katika Siku zake lakini kwa miaka ya hii wazazi wengi wamekosa muda wa kukaa na watoto wao katika kuzungumza nao mam

"Wakina mama wa sasa tumefeli kwasababu muda wa kukaa na watoto wetu hatuna ,kwa zamani mtoto wa kike anapokuwa anaingia kwenye Siku zake ,unamwambia mumeo mtoto yuko hivii mnasaidiana lakini kwa sasa imekuwa ngumu ndio maana hata sasa kuna mimba Sana za utotoni kwasababu watoto wanakosa muda wa kuzungumza na wazazi wao na Mtoto anapokuwa kwenye hedhi si jukumu la mama peke yake bali hata baba anahusika " Mama Simba

Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.