Na Mwandishi Wetu ,Dodoma.
SERIKALI imeombwa kuweka Madawati Maalum ya Huduma ya Afya kwa watu wenye ulemavu wakutosikia (viziwi) kwenye hospitali na vituo vya afya ikiwemo na miongozo ya utoaji huduma.
Rai hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa kanisa la Bethel Baptitist
Deaf Church Tanzania (BBDCT) Frenk Salungi kwenye ufunguzi wa mradi wa
kuhamasisha utolewaji wa huduma shirikishi za afya kwa watu wenye ulemavu
iliyofanyika Dodoma.
Alisema kuwa kukosekana kwa madawati na miongozo imechangia kwa
kiasi kikubwa kuwa na mazingira magumu ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa
watu wenye ulemavu hao kwa wasiosikia.(viziwi)
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mradi huo wa kanisa la Bethel
Baptitist Deaf of Tanzania (BBDCT) uliodhaminiwa na taasisi isiyo ya kiserikali
ya The Foundation for Civil Society (FCS),kwa ajili ya kukusanya maoni
mbalimbali ya namna ya kuboresha huduma za kiafya kwa wenye ulemavu ili
kuwakilisha katika mkutano na viongozi wa wizara na asasi.
Salungi alisema kuwa kukosekana kwa mawasiliano kupitia miongozo
na madawati ya afya ya watu wenye ulemavu imedidimiza na kuonekana ulemavu ni
kama ugonjwa.
“Inasikitisha makundi ya watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma,walio
wengi hawajui wajibu wala haki yao ya upatikanaji wa huduma za afya pale
wanapoumwa au kupata ajali huwa wanatapatapa hawajui pakuanzia wala pakuishia
hii yote ni kutokana na ukoefu wa madawati na miongozo ya namna ya kupata
matibabu”alisema.
Kwa upande wake Afisa muuguzi na mkunga mfawidhi
msaidizi,hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Stella Lupembe,akizungumza kwenye
uzinduzi huo wa mradi.
Alisema kuwa serikali inatambua ugumu wanaokutananao watu wenye
ulemavu wasiosikia katika kupata huduma ya afya zinazotolewa kwenye vituo
vya afya, hospitalini na maeneo mengineyo.
Alisema kuwa kutokana na changamoto waliyonayo,kuna kila sababu
watumishi mbalimbali wakiwemo wa afya kujitokeza kusoma na kuijua lugha ya
alama ili waweze kuwahudumia watu wenye ulemavu wasioona kwa kutumia madawati
na miongozo.
Hata hivyo, amewaomba wanafunzi mashuleni ambao wasiosikia
wapende kusoma masomo ya sayansi na mawasiliano ili waweze kuwahudumia jamii
hiyo pindi watakapokuwa wahudumu wa afya.
Mwisho.
Comments
Post a Comment