Na Jackline kuwanda, Dodoma.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
NHIF Mkoani Dodoma umetoa wito kwa wanafunzi wa vyuo ya Elimu ya Juu ,Kati
na Ufundi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bina ya Afya ili kuwa na uhakika wa
matibabu.
Wito huo umetolewa leo na Bakari Hamdun Afisa Uanachama na Matekelezo wa Mfuko huo Dodoma wakati
akizungumza na Mtandao wa Dodoma News Blog katika maonesho ya pili ya Elimu ya
Mafunzo na Ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta
Binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
‘’Tumekuwa tukiwapatia wanafunzi kadi
za Bima ya Afya ambazo huwatengenezea uhakika wa matibabu’’amesema Bakari
Aidha, Bakari amesema mtu akiwa na
Afya nzuri husaidia kuliletea Taifa maendeleo.
‘’ukiwa na Afya njema husaidia kushiriki
katika jitihada za kuliletea Taifa maendeleo ,Afya Bora ya leo ndiyo Afya Bora
ya kesho’’amesema Bakari
Hatahivyo, amesema wameendelea
kutoa Kadi za Bima ya Afya kwa wanafunzi wa vyuo hivyo kuhakikisha kuwa afya
zao zinakuwa bora na kukabiliana na changamoto za kiafya pindi wanapokuwa
vyuoni.
Mwisho.
Comments
Post a Comment