HALMASHAURI YA CHAMWINO YASAMBAZA MAKASHA YA KONDOMU KWENYE KATA ZAKE

 

Mmoja wa Madiwani wa halmashauri hiyo ya Chamwino akitoa npongezi zake kutokana na hatua ya kusambaziwa kwenye kata zao makasha yenya kondom kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi

DODOMA.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Chamwino kwa kushirikiana na Tume ya kudhibiti ukimwi na shirika lisilo la kiserikali la Tayoa limesambaza na kuyafunga jumla ya makasha 508 yenye kondom 10,200 kwenye kata zipatazo 25 za wilaya hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka huu.

Aidha Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakala wa barabara vijijini (TARURA) imetoa elimu ya kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi pamoja na kugawa kondom katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa barabara katika kata tatu ikiwemo ya Idifu,Nghahalezi na Manzase.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Keneth Yindi alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zilizotekelezwa na kamati ya kudhibiti ukimwi kwa kipindi cha robo mwaka  Januari hadi Machi 2020/2021,kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika wilayani Chamwino.

Alisema halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza jukumu hilo la ugawaji wa makasha hayo ya kondom, ili iweze kufikia malengo ya sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.

Yindi ambaye ni diwani wa kata ya Buigiri alitaja kata ambazo zilizonufaika na mpango huo wa usambazaji wa makasha ya kondom ni pamoja na Kata ya Nhinhi ,Mlowa Bwawani, Manzase ,Chiboli,Fufu ,Loje ,Mpwayungu na Nghambaku.

Zingine ni kata ya Chinugulu ,Huzi, Manda ,Chilonwa,Membe,Dabalo,Itis o,Segala ,Chamwino,Buigiri Msanga,Manchali,Handali,Igandu,Nghahelezi ,Mvumi Misheni na Mlowa Barabarani.

Kwa upande wa Huduma ya Tiba kwa magonjwa ya ngono na kinga kwa ajili ya kuzuia na kusambaa,alisema halmashauri imetenga vituo vipatavyo 70 na jumla ya wateja 2050 walijitokeza na kuhudumiwa ambapo kati yao wanawake 1050 na wanaume 1000.

Yindi kwenye taarifa yake hata hivyo alisema kuwa, bado kunahitajika elimu ya kutosha kwa kamati za kudhibiti ukimwi zilizopo kwenye kata kutokana na kutowasilisha kikamilifu juu ya  utekelezaji kwa kuwa hazifuatilii na kutilia athali za maambukizi ya virusi.

Hahivyo kwenye kikao hicho cha Baraza, Madiwani wa viti maalumu wameiomba halmashauri hiyo pamoja na taasisi zisizo la kiserikali kuhakikisha wanasambaza pia kondom za kike kondom za kike ili kulingika kundi hilo na maambukizi ya virusi vya ukimwi kama ilivyo kwa wanaume.

MWISHO.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.