Na Mwandishi Wetu,Dodoma.
Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Dk. Anna Makakala amewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana
na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Ndugu Alex Raphael
Kyai kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao.
Ametoa kuali hiyo jana jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi
wa habari ,amesema kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na video
fupi iliyokuwa ikisambaa mtandaoni ikiwaonyesha askari hao wakitumia
nguvu kumkamata Alex Kyai ambaye ni mtuhumiwa wa makosa ya kiuhamiaji.
Kamishina Jenerali
huyo amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu katika ofisi ya
uhamiaji kurasini Jijini Dar es Salam ambapo mtuhumiwa huyo alifika ofisini
hapo na mteja wa paspoti za uhamiaji ambaye alimtambulisha kama mke wake.
Hatahivyo,Amewataka wananchi wanaohitaji huduma za
uhamiaji kufika kwenye ofisi ili kuepusha utapeli ambao unaweza kujitokeza
dhidi yao huku onyo kwa mtu yoyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa yeye ni
afisa uhamiaji au afisa yoyote wa serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa
maslahi yake binafsi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria.
Mwisho.
Comments
Post a Comment