ACC WAHIMIZA MAZINGIRA RAFIKI KWA WATOTO WA KIKE

Na. Nemes Michael, DODOMA

Shirika la Action for Community Care – ACC, wamegawa taulo za kike, katika kata ya Mbabala Jijini hapa, wakiwa na lengo la kuwahudumia watoto wa kike kimahitaji na haswa wanao ishi katika mazingira magumu.Akizungumza katika ugawaji huo, Afisa Uborashaji Kipato kutoka shirika la ACC, Upendo Minja alieleza kuwa matazamio waliyonayo ni kuhakikisha mtoto wa kike anapata mahitaji yote muhimu kama vile taulo safi, maji safi na salama pia sehemu safi kwaajili ya kubadilisha taulo kwa wakati.

“Tarehe 28 Mei, ni siku ya Hedhi Salama Duniani tunataka kuhakikisha mtoto wa kike anapata mazingira sahii katika kujistiri na tunatazamia haswa Watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu kupitiwa na utekelezaji wa mradi wetu” alisema Minja.

Minja aliongeza kuwa Taulo za kike zilizotolewa ni taulo za kufua lakini pia kuna maelekezo katika matumizi yake na ufuaji ambapo alihimizwa wazazi kuwa msaada kwa Watoto wao katika kufuatilia maelekezo hayo.

Naye, Mratibu wa Mashauri ya Watoto kutoka ACC Susan Massawe alisema kuwa ni vyema kuhimizana katika kaya zetu kwani ndiyo mwanzo lakini pia ni njia pekee kufikia jamii yetu yote na kufanikiwa kuwatoa watoto katika mazingira magumu ili kuwajengea mazingira wenzeshi.

Kwa upande wake, Afisa Mwandikishaji Mfuko wa Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa Erick Msemwa ameonyesha kuvutiwa na mradi kutoka ACC na kuambatana nao katika kutekeleza uboreshaji wa Bima lakini pia alihimiza wanannchi kujitokeza, kujiunga pia kupokea maboresho yaliyo lenga kuimarisha uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii.  


MWISHO

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.