Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuwasilisha
taarifa za changamoto mapema ili ziweze kutatuliwa na halmashauri badala ya
kusubiri vikao.
Prof. Davis Mwamfupe |
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akifunga mkutano wa kawaida
wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji
la Dodoma.
Prof. Mwamfupe alisema kuwa madiwani wanapokumbana na
changamoto zinazohusiana na utekelezaji wa shughuli za maendeleo wasisubiri
vikao. “Karibu asilimia 75 ya hoja tulizojadili zinategemea kuwasilisha taarifa
za changamoto tofauti na kusubiri vikao” alisema Prof. Mwamfupe.
Wakili Msekeni Mkufya |
Akimkaribisha Mwenyekiti kufunga mkutano wa Baraza la Madiwani, katibu, Wakili Msekeni Mkufya aliwataka madiwani kuendelea kushirikiana na
wataalam wa halmashauri katika kuleta maendeleo ya halmashauri. “Wito wangu
kwenu, tuendelee kushirikiana kwa sababu wote tunajenga nyumba moja, kwa maana
ya kuwahudumia wananchi” alisema Wakili Mkufya.
MWISHO
Comments
Post a Comment