Na. Christina Mwagala, DODOMA
Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika dimbani la Jamhuri jijini
Dodoma kwa ajili ya mchezo wa michuano ya kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya
Dododma Jiji FC mchezo ambao utapigwa saa 16:00 jioni.
![]() |
Mchezaji wa Timu ya KMC FC, Clifu Buyogwa akiwa kwenye mazoezi kuelekea katika mchezo wa kesho wa michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Dodoma Jiji |
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Habibu Kondo amesema kuwa tayari walishafanya maandalizi ya
kutosha tangu wakiwa jijini Dar es Salaam na kwamba hana hofu katika mchezo huo
licha ya kwamba michuano hiyo ni migumu lakini anakiamini kikosi chake
kitakwenda kufanya vizuri na hivyo kuendelea katika hatua inayofuata ya
michuano hiyo ya ASFC.
Ameongeza kuwa timu anayokutana nayo kesho ni nzuri nakwamba imekuwa
ikifanya vizuri katika michezo yake ya Ligi kuu hivyo pamoja na yote bado kama
kocha na benchi la ufundi kwa ujumla watahakikisha kuwa Kino Boys inakwenda
kufanya vizuri katika mchezo wa kesho.
“Michuano hii inafahamika kabisa kwamba ukifungwa unatoka, kwahiyo
pamoja na kwamba tunakutana na timu yenye ushindani mkubwa, lakini KMC FC
imejiandaa vizuri kwasababu tunahitaji kuchukua kombe hilo awamu hii, na uwezo
huo tunao” amesema Habibu Kondo.
KMC inakutana kwa mara ya pili na Timu ya Dodoma Jiji ambao katika
mchezo wa kwanza ulikuwa ni wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo walicheza
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam na Kino Boys kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri.
MWISHO
Comments
Post a Comment