Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
WATANZANIA
wameshauriwa kufanya dua na sala ya kumwombea Rais wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan, ili aweze kukamilisha kwa wakati miradi mikubwa iliyoanzishwa na
kuachwa na aliyekuwa Rais, Dkt. John Magufuli ambayo imelenga kuwafanikisha watanzania kuwa na
maendeleo.
Rai hiyo
imetolewa Mhubiri wa kimataifa Mchungaji
Nicodemus Mganga wa kanisa la Evangelists Assemblies of God (TZ) Bagamoyo
alipokuwa akizungumza na waumini wa kanisa la Nazareth Temple Ipagala (EAGT)
Dodoma.
Mchungaji
Mganga alisema kuwa watanzania wana jukumu kubwa la kumwelekezea Mungu maombi
kwa ajili ya Rais Samia Suluhu ili aweze kukamilisha miradi iliyopo ambayo
tuliyoachiwa na aliyekuwa Rais wetu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.
Alisema kuwa
Rais Magufuli ametuachia mambo mengi ambayo yamelenga kuifanya nchi ya Tanzania
kukua zaidi kichumi,hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha tunamhezi pia kwa
kumuombea kutokana na mzigo mkubwa aliokuwanao kwa ajili ya wananchi wake.
Hata hivyo
watanzania wanatakiwa kuwa na imani kubwa na Rais Samia Suluhu ukizingatia kuwa
yeye ndiye aliyekuwa makamu wake kwa maana hiyo yale yote aliyokuwa akifanya
Rais Magufuli kwa upande wake atafanikisha tena kwa spidi kubwa.
Awali
akizungumza na waumini Askofu mstaafu, Dkt. Evance
Chande amewataka watanzania kufanya kazi kwa juhudi kubwa,ikiwemo na ulipaji
kodi ili Tanzania ifanikiwe kwenye malengo yake ya kuwafikishia watanzania
maendeleo yao.
Dkt. Chande alisema kuwa hakuna sababu ya kukaa bila kufanya kazi na
ukwepaji wa kodi,kinachotakiwa kuiunga serikali ambayo imekuwa mstali wa mbelel
katika kuhakikisha watu wake wanaondokana na umasikini usiokuwa na tija.
Askofu huyo
mstaafu alisema watanzania wakishiriki kwa uaminifu katika kufanya kazi na
kulipa kodi, serikali iliyopo chini ya Rais Samia Suluhu itakuwa namaendeleo
ambayo yatakayoenda kwa haraka na wepesi kwa kuwafikia watu bila kujali itikadi
yoyote.
MWISHO
Comments
Post a Comment