Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
Wito
umetolewa kwa Watanzania kuendelea kumwamini Mungu aliyewaumba wanadamu wote
hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linapitia katika msiba mkubwa na mzito
wa kuondokewa na Kiongozi Mkuu wa Taifa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Wito huo umetolewa na Katekista Yonah Kusaja wa Kanisa la Aglikana Parish ya Mtakatifu, Stephano-Kikombo Jijini Dodoma wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wetu ambapo amesema kuwa,Mungu alitupa Kiongozi huyo kama zawadi, hivyo ni yeye pia ndiye aliyeamua kutunyang’anya zawadi hio.
Ametoa wito
kwa Watanzania kuyaishi mambo mema yaliyo asisiwa na Hayati Rais, Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli, sanjari na kuendelea kumtegemea Mungu katika kila jambo kama
ambavyo Marehemu alikuwa akisisitiza enzi za uhai wake.
Hata hivyo
Katekista Kusaja amemuomba Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu
Hasani kwa nafasi yake kuyaendeleza mambo mema aliyoyaanzisha mtangulizi wake
na kuyakamilisha kwa wakati.
Kwa upande
wake Mchungaji Paniel Nnko wa Kanisa la Christian Center Miyuji Jijini Dodoma
amesema kuwa, Taifa
limempoteza Kiongozi mzalendo ambaye aliyatoa maisha yake yote kuhakikisha
anaongoza mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na
uzembe kazini.
Aidha, Mchungaji Nnko amewamba Wakristo na
Watanzania wote kwa ujumla kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha maombolezo
liwe na amani na utulivu, huku nae akimuomba Rais Samia na Viongozi wote
serikalini kuwatumika vyema Watanzania kwa kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza,
kutenda haki na kuweka uzalendo mbele.
MWISHO
Comments
Post a Comment