WALIYOYASEMA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA WALIOFIKA KUMUAGA HAYATI RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UWANJA WA JAMHURI JIJINI DODOMA
Kuondoka kwa Dkt. John Pombe Magufuli kumetikisa bara la Afrika. Bara la Afrika "linajikuta hayati" kwa kupoteza mwanasiasa mkongwe na kiongozi aliyelenga kuboresha maisha na kulinda maslahi ya wananchi wake - Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Tutabaki na
kumbukumbu ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kama Mpiganaji na Mzalendo. Sio tu
kwa watu wa Tanzania bali kwa Afrika nzima, mtetezi mkuu wa Uhuru wa
kiutamaduni na kiuchumi wa bara la Afrika - Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo
Sisi kama Wakenya
na mimi binafsi, tulisema lazima tuje kumsindikiza ndugu yetu. Tutaendelea
kufanya kazi pamoja na kushirikiana na hatimaye kuleta Jumuiya ya Afrika
Mashariki na Bara la Afrika Pamoja – Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Tumeona kazi ya
barabara, tumeona kazi ya umeme, tumeona kazi ya ujenzi wa viwanja vya ndege na
miradi mingine mingi ambayo itaenda kuleta manufaa kwa Watanzania na manufaa
kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukuza biashara. – Uhuru Kenyatta, Rais wa
Kenya
Niko hapa kumuomboleza
rafiki wa karibu, mtu ambaye tuliongea mara kwa mara tukibadilishana mawazo
kuhusu nchi zetu na Jumuiya ya Afrika Mashariki - Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Leo Afrika
imepoteza mtu mashuhuri, leo wananchi wa Tanzania wamempoteza raia muaminifu,
mfanyakazi na mwenye Imani ya kipekee iliyokuza taifa la Tanzania na bara la
Afrika - Mhe. Felipe Nyusi, Rais wa Msumbiji
Utulivu wa kisiasa
wenye sifa nzuri na za wazi, ustawi wa kijamii na kiuchumi wa Tanzania,
miundombinu ya msingi kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha ya Watanzania,
viwango vya juu vya ufanisi na utendaji bora wa Serikali ni matunda ya uongozi
wa Rais Magufuli - Mhe. Felipe Nyusi, Rais wa Msumbiji
Umoja wa Familia ya
Afrika leo unaomboleza kwa kuondokewa na kiongozi mahiri ambaye alikua na maono
ya kulikomboa bara la Afrika. Tumempoteza mtetezi wa Afrika aliyesimama bila
uoga kulitetea bara la Afrika - Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika
Kusini
Bado nakumbuka Rais
Magufuli alivyokuja Afrika Kusini wakati naapishwa na akanipa maono na dira
aliyonayo kwa nchi ya Tanzania na watu wake. Nilifarijika sana kwasababu Rais
Magufuli hakuwa mtu wa kusafiri sana, alipendelea kukaa nchini kwake - Cyril
Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini
Serikali na
wananchi wa Visiwa vya Comoro tunatuma salamu za rambirambi kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Mama Samia. Kuondoka kwa Dkt. John Pombe
Magufuli ni pigo kubwa sana kwa bara la Afrika, dunia na kwa Visiwa vya Comoro
- Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani
Nchi ya Comoro ipo
kwenye msiba mkubwa sababu Comoro na Tanzania ni kitu kimoja na vitu vinavyo
tuunganisha ni vingi ikiwemo historia, jiographia, lugha na malengo yote yenye
nia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wetu. Bara la Afrika limepoteza mtu mkubwa
sana aliyeweka bara hili mbele - Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani
Miezi kadhaa
iliyopita, mimi na Rais Magufuli tulipata chakula cha jioni Ikulu Dar es
salaam, sikufahamu kuwa ndio ingekua mara ya mwisho kukaa naye na kupata
chakula cha jioni. Alinisindikiza mpaka kwenye uwanja wa ndege, lakini sikijua
kama ndio ingekua mara ya mwisho kuonana - Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera
Waliosema wala
rushwa na wanaokandamiza Serikali na nchi za Afrika hawawezi kukabiliwa
hawakutegemea Magufuli angesimama kidete kupambana nao, waliosema nchi za
Afrika haziwezi kuingia uchumi wa kati katika kipindi cha muhula mmoja wa
uongozi hawakutegemea Magufuli angefanikisha hilo - Rais wa Malawi, Lazarus
Chakwera
Rais Magufuli
alikuwa rafiki yangu wa karibu sana na nitamkumbuka sana. Maombi yetu tunatuma
kwa familia na wananchi wote wa Tanzania. Tunaomba mwenyezi Mungu awapunguzie
majonzi na kuwapa nguvu katika kipindi hichi kigumu – Rais wa Zambia, Edgar
Lungu
Siku ya leo ni siku
ya giza sana hapa Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla. Sisi watu wa Zimbabwe
tuliumia sana sababu Rais Magufuli alijitoa kuitumikia Tanzania na Bara la
Afrika - Emmerson Mnangagwa, Rais wa Zimbabwe
*Imeandaliwa na
IDARAYA HABARI MAELEZO*

Comments
Post a Comment