Makala imeandikwa na Albano Midelo, Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
LICHA
ya kwamba mengi yameandikwa kuhusu kiwanja cha ndege cha Songea kilichopo
Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,bado kuna mengi yanayokihusu kiwanja
hiki.
Ndege ya ATCL yenye ujwezo wa kubeba abiria 76 ikiwa imetua kwenye kiwanja cha Songea baada ya kurejeshwa safari kuanzia Februari 17 mwaka huu |
Historia
inaonesha kuwa kiwanja cha ndege cha Songea kilianzishwa mwaka 1950 ambacho
kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi aliyefahamika kwa jina moja la Robert.
Meneja
wa Kiwanda cha Ndege Songea Jordan Mchami anasema ilipofika mwaka 1963 serikali
ilichukua umiliki wa, kiwanja hicho kutoka kwa mtu binafsi na kuanza
kukiendesha kiwanja hicho.
Hata
hivyo anasema wakati serikali inakichukua kiwanja hicho,barabara ya ndege
ilikuwa ni ya vumbi na kwamba ilipofika mwaka 1979,serikali iliona umuhimu wa
kukikarabati kiwanja hicho kwa kukiwekea lami.
“Wakati
serikali inakarabati kiwanja hicho kwa kukiwekea lami ,barabara ya ndege
ilikuwa na urefu wa meta 1625 na upana wa meta 30,uwanja uliendelea kutumika
kwa kutumia ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba abiria 13’’,anasema Mchami.
Jengo la kukaguliwa abiria kabla ya kuruhusiwa kuingia uwanjani |
Kwa
mujibu wa Meneja huyo, ilipofika mwaka 2017, barabara ya ndege katika kiwanja cha
Songea ilikuwa imechakaa sana hivyo serikali iliona umuhimu wa kukarabati
kiwanja hicho kwa kuongeza urefu wa barabara ya kuruka na kutua ndege toka
urefu wa awali wa meta 1625 kwa upana wa meta 30 na kufikia meta 1740 ambapo
upana wake ulibakia meta 30.
Kwa
upande wake Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Lasack Alinanuswe anasema
ukarabati wa kiwanja hicho. umetekelezwa na kampuni ya CHICCO kutoka nchi ya
Jamhuri ya China na kusimamiwa na Wakala wa Barabara TANROADS kwa gharama ya
shilingi bilioni 37.
Anazitaja
kazi ambazo zimehusika kwenye ukarabati
na upanuzi wa kiwanja hicho kuwa ni urefushaji wa barabara ya kutua na
kuruka ndege kutoka meta 1625 hadi meta
1740.
Hata
hivyo anabainisha kuwa mwisho wa pande zote za kutua ndege kuna eneo la usalama
(Stop way) lenye urefu wa meta 60 kila upande hivyo kufanya barabara yote kuwa
na urefu wa meta 1860
Kulingana
na Meneja huyo wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma,maeneo mengine yaliyokarabatiwa ni eneo la maegesho madogo ya ndege yenye ukubwa
wa meta 70 kwa meta 40 na kwamba matumizi ya maegesho hiyo ndogo ya ndege ni
kuegesha ndege za dharura na ndege za kijeshi.
Meneja Kiwanja cha Ndege Songea Jordan Mchami akitoa historia ya kiwanja hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1950 |
Mhandisi
Alinanuswe anasema katika kiwanja hicho kumejengwa maegesho kubwa ya ndege
yenye uwezo wa kuegesha ndege sita kubwa aina ya bombardier kwa wakati mmoja
yenye urefu wa meta 139 na upana wa meta 126.
Hata
hivyo anasema maegesho ya ndege ya zamani ilikuwa ni ndogo yenye urefu wa meta
72 kwa meta 55 na kwamba katika ukarabati huo,limejengwa jengo jipya kwa ajili
ya abiria lenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 150 hadi 200 ambapo jengo la
zamani la abiria lilikuwa na uwezo wa kuhifadhi abiria 75 tu.
Meneja
Kiwanja cha Ndege Songea,anazitaja fursa zilizopo katika kiwanja hicho kuwa
ni maeneo ya kupangisha wawekezaji kwa
ajili ya kuweka maduka,hoteli pia kuna maeneo ambayo kiwanja cha ndege Songea kinaweza
kuingia ubia kwa kutoa ardhi na wawekezaji kujenga na baada ya kumaliza mkataba
eneo linabaki kuwa mali ya kiwanja cha ndege.
Anaitaja
fursa nyingine inayopatikana kwenye kiwanja hicho,ni fursa ya biashara ya taksi
kwa ajili ya kusafirisha abiria toka katika kiwanja cha ndege hadi mjini
Songea.
Akizungumzia
mwenendo wa abiria tangu kurejeshwa kwa safari za abiria za ndege za ATCL
Feburiari 17 mwaka huu,Meneja Kiwanja cha Ndege Songea anasema mwitikio wa
abiria ni mzuri kwa sababu ndege iliyokuwa inatoa huduma kabla ya ATCL ilikuwa
ni ndogo yenye uwezo wa kubeba abiria 13 tu na nauli yake kwenda pekee ilikuwa
ni zaidi ya shilingi 500,000.
“Hivi
sasa kupitia ndege ya serikali za ATCL yenye uwezo wa kubeba abiria 76, nauli
kwenda tu ni shilingi 250,00, kwenda na kurudi ni shilingi 370,000 kwa hiyo
abiria wamepunguziwa mzigo wa nauli’’, anasema Mchami.
Anasisitiza
kuwa kutokana na hali hiyo siku hadi siku idadi ya abiria inaendelea kuongezeka
ambapo hivi sasa ratiba ya ndege ni mara mbili kwa wiki,siku za Jumatano na
Jumapili ambapo uzoefu unaonesha kuwa siku ya Jumapili kunakuwa na idadi kubwa
ya abiria.
“Tunatarajia
kuwasiliana na ATCL Makao makuu kuona uwezekano
wa kubadilisha ratiba ya ndege ikiwezekana iwe siku za Jumatatu,Jumatano
na Ijumaa ili Ijumaa jioni watu wanaweza
kutoka kazini kuamua kusafiri na Jumatatu Asubuhi kurejea kazini Songea, kwa
kifupi idadi ya abiria inaridhisha’’,anasisitiza Mchami.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme anasema kiwanja cha ndege wa Songea ni
rasilimali adimu inayoweza kusaidia kukuza uchumi wa mji wa Songea na Mkoa
mzima wa Ruvuma hasa kukuza sekta ya utalii,baada ya kuanzishwa mpango mkakati
wa kukuza utalii katika mkoa wa Ruvuma.
Comments
Post a Comment