SERIKALI YAANZISHA TAHSUSI MPYA TANO

Na. DOTTO KWILASA, DODOMA

 

SERIKALI imetangaza kuanza kwa tahsusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato Cha tano mwaka huu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini.


 

Waziri Selemani Jafo

Tahsusi hizo ni Physics, Mathematics na Computer Studies (PMC), Kiswahili, French, Chinese (KFC), Kiswahili, English, Chinese (KEC), Physical education, Biology, Fine art (PeBFa) na Physical education, Geography, Economics (PeGE).

 

Hayo yameelezwa jana Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

 

Jafo alisema tahsusi ya PMC kwa kuanzia itatolewa katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Dodoma na Shule ya ufundi ya wavulana ya Iyunga Mkoani Mbeya.

 

Aidha, alisema tahsusi ya PeBFa na PeGE itatolewa shule ya Sekondari ya wasichana ya Makambako, shule ya Sekondari ya wavulana Kibiti na Sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.

 

Akizungumzia utaratibu wa kubadilisha tahsusi na vyuo vya ufundi kwa Mwaka 2021 Waziri Jafo alisema ratiba ya kubadili inaanza Machi 29 hadi Aprili 11,2021.

 

Pamoja na mambo mengine Waziri Jafo alitoa wito kwa wanafunzi kutumia muda uliowekwa vizuri kuweza kubadili tahsusi kwa njia ya mtandao kulingana na ufaulu Waliopata kwa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kufanya uchaguzi mwingine tena, isipokuwa taarifa za awali ndizo zitakazotumika.

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.