SERIKALI ITAHAKIKISHA UPATIKANAJI WA DAWA UNAKUWA WA KURIDHISHA

Na. Catherine Sungura. WAMJW, Dodoma

 

Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya unakuwa wa kuridhisha.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara  katika kipindi Cha Julai 2020 Hadi Februari 2021 iliyobarilishwa Kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii


Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara (Idara Kuu ya Afya) kwa kipindi Cha Julai 2020 Hadi Februari, 2021 Kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema katika kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa wakati na zenye ubora,Serikali ilitenga kiasi Cha shilingi Bilioni 200 katika kipindi Cha mwaka 2020/2021 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa aina 312 za Dawa upatikanaji umefikia kiasi Cha asilimia 74.

Hata hivyo amesema Wizara ya Afya imeboresha huduma za afya ya uzazi nchini katika kipindi Cha Julai 2020 Hadi Februari 2021 ambapo jumla ya wajawazito 1,165,526 (sawa na asilimia 103 ya waliotarajiwa) walihudhuria kliniki na kupata huduma.

Kaimu Katibu Mkuu-Idara Kuu ya Afya Edward Mbanga akitoa ufafanuzi wakati wa kuwasilisha taarifa ya Wizara


"Kati ya wajawazito hao asilimia 36.5 ndio walianza huduma kabla ya wiki 12 ikilinganishwa na asilimia 36.4 kipindi Kama hiki mwaka 2019".

Aliongeza kuwa asilimia 90.4 walifanya mahudhurio manne au zaidi ikilinganishwa na asilimia 84.1 mwaka 2019.

Kwa upande wa waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya, Dkt. Gwajima amesema wajawazito 920,126 sawa na asilimia 82 Kama ilivyokua katika kipindi Kama hicho mwaka 2019.

Aliongeza kuwa katika kuimarisha huduma za Kinga hususan huduma za Chanjo jumla ya Watoto wa chini ya mwaka mmoja 1,030,617 walitegemewa kupatiwa chanjo kwa ajili ya kuwakinga na Magonjwa mbalimbali na Hadi kufukia Februari 2021 Watoto 1,010,005 sawa na asilimia 98 walipatiwa chanjo kwa kutumia kigezo Cha PENTA-3 kwa mujibu wa mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.