MAELEZO MAFUPI YANAYOMUHUSU MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGAMO WA TANZANIA DR. PHILIP ISIDORY MPANGO
Dk Philip Mpango
ametokea katika nafasi ya Waziri wa Fedha na Mipango katika
Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la
Rais John Magufuli. Alikuwa ni mbunge katika jimbo la
Buhigwe mkoani Kigoma ambapo Katika uchaguzi uliopita wa
Octoba 2020 Dkt Mpango alipita bila kupingwa.
Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapo hapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.
Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alikuwa akifundisha “Microeconomics”, “Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili ambayo ni Uchumi mdogo, Uchumi mkubwa na masuala ya Fedha za umma.
Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.
JPM alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.
Ni kiongozi mwenye dira na maono mapana, ni mtendaji anayeweza kusimamia jambo alilokabidhiwa na likafanikiwa. Alipoteuliwa kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, ndani ya mwezi mmoja ukusanyaji wa mapato wa taasisi hiyo ulivunja rekodi. Kwa mara ya kwanza TRA ilikusanya zaidi ya Sh1.4 trilioni kwa mkupuo. Rais JPM alijitokeza na kumpongeza kwa hatua hiyo na muda mfupi baadaye akamkabidhi Wizara ya Fedha.
Philip Mpango alizaliwa Julai 14, 1957 ni alikuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania akiwa ofisini tangu Machi 2015. Mpango hapo awali alishikilia nafasi kama kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), [3] katibu mtendaji katika Ofisi ya Rais (Tume ya Mipango), naibu katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, msaidizi binafsi wa rais (masuala ya uchumi), mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Kiuchumi wa Rais, na kama mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia.
Mara baada ya kuteuliwa jana machi 30,2021 katika Mkutano wa tatu kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais jimbo la BUHIGWE limetangazwa na spika wa Bunge hulio Job Ndugai kuwa lipo wazi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment