Na Jackline Kuwanda,Dodoma.
Serikali kupitia
Wizara ya Kilimo imegawa vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi Milioni mia
mbili arobaini na mbili ,elfu sitini na sita,mia tisa hamsini na tisa na senti
thelathini (242,66,959.30) kwa vyuo 29
vya kilimo.
Akizungumza
wakati wa kugawa vifaa hivyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gelard Kusaya amesema ili
kufanikisha mafunzo kwa njia ya mtandao yanatolewa ni muhimu kuwa na vifaa vya
kisasa na vyenye uwezo .
Aidha Kusaya
amesema vyuo vya mafunzo ya kilimo ni
kitovu cha kuzalisha wataalamu wa kilimo
kwa lengo la kutoa maarifa na ujuzi kwa wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija
na kujiongezea kipato.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo cha Karuc Afra Rwechungura ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya
kilimo kwa kutambua mchango wa vyuo visivyo vya kiserikali katika kufundisha na
kutoa wataalamu katika kilimo .
Naye Mkuu wa Chuo
cha Mlingano Mhandisi Samson Cheyo amesema kupitia vifaa hivyo vitasaidia kwenda
kuboresha utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi kwa njia za kisasa ili kutoa
wataalamu wanaoweza kuajirika hapa nchini.
Mwisho.
Comments
Post a Comment