DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Taasisi ya Alhikma
inayoandaa mashindano ya Qur-an Afrika Sheikh Nurdin Kishk amesema taasisi hiyo
itamkumbuka Hayati Magufuli kwa mchango wake ikiwemo kutoa eneo lenye ukubwa wa
hekari moja na nusu kwa shirika hilo kwa ajili ya kujenga eneo kubwa la ibada
Hayati Dkt John Pombe Magufuli
atakumbukwa kwa mengi hasa katika mchago wake wa kuhakikisha taasisi za kidini
zinafanya kazi zake kwa uhuru bila wasiwasi na wakati fulani ilishuhudiwa
akiongoza harambee iliyolenga kujenga msikiti jijini Dodoma pia aliwahi kutoa
eneo lenye ukubwa wa hekari moja na nusu kwa taasisi ya Alhkma kwa ajili ya
kuendeleza kutoa mafunzo ya kumjua Mwenyezi Mungu
Katika hatua nyingine Taasisi
hiyo imetambulisha mashindano ya 21 ya Qur-an tukufu Afrika yatakayofanyika April
25 mwaka huu ambapo siku hiyo pia itatumika kusoma dua Maalum ya kuliombea
taifa juu masuala mbalimbali ikiwemo kuliombea Taifa juu liepushwe na magonjwa
mbali mbali
Sheikh Nurdin Kishk pia
amewasihi watanzania kumuunga mkono Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan ili aweze kuendeleza kazi iliyoachwa na hayati Dkt
John Pombe Magufuli.
Comments
Post a Comment