CHIFU MAZENGO WA PILI DODOMA AWAASA WATANZANIA KUWA NA UMOJA KIPINDI HIKI AMBACHO NCHI INAOMBOLEZA KIFO CHA HAYATI DKT MAGUFULI

 


Na Jackline Kuwanda,Dodoma.

Chifu Mkuu wa  Kanda ya kati Mtemi Mazengo wa pili ametoa wito kwa watanzania kuzingatia umoja na ushirikiano katika kipindi hiki ambacho nchi imempoteza kiongozi shupavu na mzalendo aliyeipenda nchi yake na kujali watu wake katika kutekeleza mapinduzi makubwa ya uchumi wa wananchi wa Tanzania.

Wito huo ameutoa leo wakati akizungumza na Mtandao wa Dodoma News Blog,ambapo amesema Hayati Dkt John Pombe Magufuli atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwemo kuibadili Taswira ya Tanzania kwa kumtegemea Mungu katika mipango na mikakati ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa.

Aidha, amesema Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa aliyoiheshimisha kwa kuacha alama  nyingi ikiwemo kuipa hadhi ya kuwa jiji,miundombinu kuboreshwa,hospitali kujengwa,shule kujengwa ’’kiukweli amefanya mambo mengi ameacha kumbukumbu kubwa sana katika Mkoa wa Dodoma na hata sisi machifu ametuheshimisha kwa kurejesha nafasi zetu tena’’ Mazengo Amesema

Wakati huo huo Mazengo amesema hali ya machifu kurudishwa katika uongozi kwao ilikuwa ni heshima kubwa kutoka kwa kiongozi huyo.

Katika hatua nyingine amesema kwa kiongozi wa sasa aliyepo Madarakani Rais Mama Samiah Suluh Hasan wao kama machifu wanamuombea kwa mwenyezi Mungu kuyaendeleza yale ambayo Hayati Dkt Magufuli aliyaacha.

Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Pombe Magufuli alifariki Dunia Machi 17/2021 baada ya kugua maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 61.

Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.