Na. Joyce Kasiki, MAKETE
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametembelea
kwenye milima ya Kisajanilo wilayani Makete kwa ajili ya kufuatilia chanzo
cha mradi wa Maji ya Ilolo-Bulongwa na kuahidi kutoa sh. milioni 309 kwa ajili ya kuukamilisha
mradi huo ili uanze kutoa maji.
Katibu
Mkuu huyo akiwa ameongozana na mbunge wa Makete Festo Sanga katika mradi huo
ulioibuliwa na wananchi mwaka 2018 na ametanguliza kiasi cha shilingi milioni
100 na kutoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) mradi huo uanze
kufanya kazi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea chanzo hicho cha maji Mhandisi Sanga amewapongeza wananchi kwa kuibua chanzo hicho cha maji lakini pia amempongeza Mbunhe wa Jimbo hilo ambaye amekuwa akifuatilia suala hilo mara kwa mara Wizarani ili Serikali iunge mkono juhudi hizo za wananchi na waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
"Rais anawapongeza kwa jitihada za kuibua miradi na kutumia nguvu zenu kuianzisha,mmeanzisha mradi huu
miaka
miwili imepita, Mbunge amenisumbua sana na nimefanya naye vikao zaidi ya mara
tatu juu ya hali ya maji Makete na nimeamua kufika hapa ili tushughulikie
changamoto za maji"alisema Mhandiai Sanga na kuongeza kuwa
"Serikali ni sikivu na ninawaagiza RUWASA ndani ya siku 60 mradi huu ukamilike, jumanne (kesho kutwa) tutaleta milioni 100 za kuanzia"
Mbali na kutembelea mradi huo pia Katibu Mkuu huyo akiongozana na Mbunge wa Jimbo hilo watatembelea kata ya Lupila, Tandala na Lupalilo kwa ajili ya kuangalia miradi ya maji.
MWISHO
Comments
Post a Comment