Na. rEVOCATUS kASSIMBA, Wizara ya Kilimo
Wananchi wa wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro
wameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua kudhibiti makundi ya nzige
waliovamia maeneo ya mashamba ya kufuatia zoezi la kuangamiza nzige hao
waliovamia mashamba yao hivi karibuni.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo baadhi ya
wakulima walimweleza Naibu Waziri wa
Kilimo Hussein Bashe aliyetembela mashamba ya Nanai eneo la Sanya Juu wilaya ya
Siha kufuatilia kazi ya kuangamiza nzige ikiwa ni leno la serikali kulinda maisha ya watu na
mali zao.
Mzee Felix Mosha mkulima na mmiliki wa shamba la
Kafori West Kilimanjaro alisema tukio la kuvamiwa na nzige juzi lilileta
taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kuwa sasa ndio wameanza kupanda mazao
mashambani lakini wamefarijika kuona hatua za serikali chini ya wizara ya
Kilimo kuwadhibiti nzige hao.
“Tunaishukuru serikali kwa kuja kwa haraka, leo
tumeona wataalam wamefanikiwa kuwaangamiza nzige waliovamia mashamba yetu ya
makademia na ngano yanaendelea kuwa
salama” alisema Mzee Mosha.
Naye mkulima Hassan Gonga anayemiliki shamba la Nanai wilaya ya Siha alisema mara baada ya wadudu hao kuvamia shamba lake la makademia waliwatafiti wadudu hao na kugundua kuwa hawapendi kelele hivyo wakaweka vifaa vya kupiga kelele shambani hapo hali iliyosababisha nzige hao waondoke kwenda msituni na kuliacha shamba likiwa salama bila madhara.
Akizungumzia operesheni kuangamiza nzige, Naibu
Waziri Kilimo Hussein Bashe alisema mpaka sasa hali ya kuangamiza nzige tangu
walipovamia maeneo ya Tanzania inaendelea vizuri na wadudu wamedhibitiwa kwa
kupuliziwa viuatilifu kuwaua kwa njia ya
ndege na mabomba ya kushikwa kwa mikono.
Bashe alisema
kuwa wizara inatambua wilaya ya Siha ni muhimu kwa kilimo hivyo lazima
itazamwe kwa karibu nzige wasije haribu ndio maana wanaendelea kwenda kujionea
kazi ya kuwadhibiti nzige hao ambapo ameshuhudia makundi ya nzige waliokufa
baada ya kupuliziwa sumu.
Bashe aliongeza kusema wizara imeongeza vifaa vya
kusaidia kupambana na nzige pia imeanzisha mafunzo kwa maafisa ugani wa vijiji
na kata kutambua aina za nzige ili iwe rahisi kudhibiti pale watakapojitokeza
kwenye maeneo yao
“Mpaka sasa Longido tumefanikiwa kwa asilimia 95
zoezi limefanikiwa hakina masalia ya nzige ambapo nzige waliovamia Siha
walitokea Longido baada ya kundi lao kupuliziwa sumu hivyo wakakimbia na sasa tumewafuata hapa
Sanya Juu tumewaua? Alisema Bashe.
Bashe aliongeza kusema kazi ya kudhibiti nzige
wilaya ya Simanjiro imeenda vizuri ambapo hadi sasa taarifa za wataalam
zinaonesha kumebakia kundi moja lililolojificha kwenye milima na kazi ya
kulifuatilia ili liangamizwe.
“Hadi sasa hakuna madhara yoyote kwenye mazo ya
wakulima tanagu nzige wavamie nchi hapa mwezi Janauri mwanzoni. Ni heri tupate
madhara ya kufa kuku lakini nzige lazima tuwatafute kokote waliko “ alisisitiza
Waziri Mkenda
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia za
visumbufu Taasisi ya Udhibiti wa Viautilifu kwenye Ukanda ywa Kitropiki (TPRI)
Mhandisi Julius Mkenda alieleza kuwa kundi la nzige lililovamia wilaya ya Siha
ni baadhi ya waliokimbia Longido baada ya kazi ya kunyunyizia kiuatilifu tarehe
22 mwezi huu hivyo wakatoroka na kuingia Siha na kuwa siyo kundi jipya kwa
mujibu wa utafiti waliofanya.
Mhandisi Mkenda alibainisha kuwa nzige waliovamia
Siha wanaendelea kuangamizwa kwa kutumia ndege maalum pia mabomba ya kupuliza
kwa miko kwa wale walio jirani na makazi ya watu ambapo zoezi limeenda vema
jana na leo na kuwa wataendelea kuchukua hatua za kuwadhibiti .
“Jambo kubwa kwa Siha ni kuwa nzige hawa wana siku
tatu tayari wameanza kuwa wa njano toka wekundu hali amabyo ni hatari hivyo sasa tunawafundisha maafisa
ugani wa kata na vijiji wajue namna ya kuwatambua na kuwadhibitipindi
wakijitokeza tena” alisisitiz Mhandisi Mkenda.
Waziri wa Kilimo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo
wapo kwenye mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kufanya ufuatiliaji wa karibu wa
udhibiti wa makundi ya nzige ili wasije haribu mashamba ya wakulima.
Mwisho
Comments
Post a Comment