JESHI la kujenga Taifa (JKT) limetia saini mkataba wa maridhiano na Wizara ya Kilimo wenye lengo la kuhakikisha Taifa linapata chakula cha kutosha.
![]() |
Kushoto ni katibu mkuu wizara ya kilimo, Gerald kusaya na kulia ni meja generali Charles mbuge mkuu wa Jshi la Kujenga Taifa |
Akizungumza leo Jijini hapa Mkuu wa Jeshi la
kujenga Taifa JKT Meja Generali Charles Mbuge amesema mashirikiano hayo yana
lengo la kulinufaisha taifa kwani Taifa likiwa na njaa shughuli za
kiuchumi haziwezi kufanyika.
Aidha Meja Generali Mbuge amesema kilimo ndio uti
wa mgongo ambapo kwa Tanzania Kilimo kinahusisha matabaka yote wenye
kipato na wasio na kipato
"Makubaliano hayo Kati yaJeshi la kujenga
Taifa (JKT) yamekuja wakati muafaka kwani vijana wengi wa Tanzania wamekua
wakijitolea kwenye mafunzo hivyo wakiwa ndani ya JKT watapatiwa mafunzo ya
Kilimo ambapo na wao wataenda kuitumia vizuri pindi wawapo uraiani.
Na nakuongeza kusema kuwa "Jeshi ni chombo
pekee ndani ya Taifa letu hivyo endapo likitumiwa vizuri litaleta manufaa makubwa
katika Taifa"amesema
Hata hivyo amesema JKT imeshaanza shughuli za
Kilimo kwa mazao ya kimkakati Katika maeneo mbalimbali ya hapa Nchini.
Naye Kanali Hassan Mabena ambae ni Kaimu Mkuu wa
utawala Jeshi la kujenga taifa (JKT )amesema lengo la kuwekeana saini ni
kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kulipunguzia Taifa mzigo.
"Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limejiwekezea
nguvu kubwa katika vikosi vyake kwani mazao yote ya kimkakati yanalimwa
Katika vikosi hivyo"
Aidha amebainisha changamoto wanazokumbana
nazo katika Kilimo ni mabadiliko ya tabia nchi, na uhaba wa pembejeo za Kilimo.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya
amesema makubaliano hayo yalikua ni ndoto yake ya kila siku kwani yeye ni
mfatiliaji mkubwa katika shughuli wanazo fanya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
kukutana kwao na kutiliana saini ni moja wapo ya
Malengo Makubwa kwani JKT shughuli za kilimo wanazo fanya zinajulikana ila
wizara ya kilimo ndio vinara.
MWISHO
Comments
Post a Comment