Jafo azitaka mamlaka za maji nchini kuweka miundombinu rafiki kwa Jeshi la zimamoto

Na. Rhoda Simba, DODOMA 

WAZIRI wa Nchi Ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleimani Jafo, amezitaka Mamlaka za Maji Nchini kuweka miundo mbinu ya maji kwa wingi ili iwe rahisi kwa Jeshi la Zimamoto kupata huduma ya maji pindi wananchi wanapokumbwa na majanga ya Moto.

 

Waziri Selemani Jafo

Kauli hiyo ameitoa leo jijini hapa kwenye uzinduzi wa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama Cha Skauti Tanzania.

Waziri Jafo amesema Jeshi la Zimamoto limekuwa likijitoa kufa na kupona Katika kuhakikisha tu,pale wananchi wanapopatwa na majanga ya Moto wanasaidiwa kwa weledi na wakati licha ya lawama nyingi kupata kutoka kwa wananchi.

"Leo nimepata furaha Sana baada ya kuona kwamba miundombinu yetu hasa ya shule inaenda kunusulika na kwakufanya hivi tutapunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya majanga ya Moto ya mara kwa mara mashuleni kwani makubaliano Haya hakika ni mafanikio makubwa ,".

Na kuongeza "Huu ni mwanzo mpya kwani tunakwenda kusaidia Taifa letu hasa katika miundombinu yetu ya shule bila kusahau serikali inamtumia mabilioni ya Fedha kujenga na kukarabati shule na Mwisho wa siku kuteketea kwa moto," amesema Waziri Jafo.

Amesema makubaliano hayo Kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama Cha Sikauti ni njia bora kwani na wao watakwenda kuwafundisha Vijana wenzao huko mashuleni mbinu za awali za kujikinga na majanga ya Moto.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Khamis Hamza amesema kwa hivi karibuni matukio ya Moto yamekithiri hali inayopelekea wengine kupoteza maisha,kupata ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza mali zao.

"Licha ya kuwepo kwa matukio hayo ya mara kwa mara jeshi la zimamoto nchini limeendelea kuchukua hatua mbalimbali  kama kujenga visima vya Dharura,na kutoa elimu ya majanga ya moto kwa wananchi,"

Na kuongeza "Na leo niseme tu ni jambo jema kwani mashirikiano Kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama cha Sikauti kwa kuwapa elimu ya  kupambana na majanga ya Moto kwa njia ya awali hakika tunakwenda kulidhibiti suala hili," amesema Hamza

Kwa Upande wake skauti Mkuu Mwantumu Mahiza amesema Skauti Tanzania kwakutambua kwamba Serikali inamtumia gharama kubwa katika kujenga na kukarabati Shule na ndio Maana  wameridhia makubaliona hayo Kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama Cha Skauti Tanzania.

Aidha, amesema chama cha skaut kimekua kikijishughulisha katika majanga ambavyo yamekuwa yakitokea nchini kusaidia na kuokoa uhai na mali za wananchi. 

"Hivyo basi makubaliano Haya Kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama cha Skauti ni mafanikio makubwa katika kuhakikisha mali za shule zinanusurika na majanga ya Moto. 

 

MWISHO

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.