Na. Mwandishi Wetu,
Waziri wa Viwanda
na Biashara, Mhe. Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini
na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na
kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.
Akizungumza na na wazalishaji hao leo jijini Dodoma Mhe. Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji
wenye tija kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.
”Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua
changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia
kazi” amesema Mhe. Mwambe.
Hata hivyo Mhe. Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali
itashughulikia changamoto hizo ili kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji
zaidi nchini.
Awali Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Geoffrey Mwambe, amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja
wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania, Bw. Abdullahi Baba.
MWISHO
Comments
Post a Comment