SERIKALI YATAHADHARISHA UGONJWA WA KICHOCHO

Na Saleh Ramadhani

 

Kaimu Mganga Mkuu Wa Serikali, Dkt. Saitor Laiza amebainisha kuwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na watu wenye umri wa kati wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maabukizi ya ugonjwa wa kichocho.

Hayo yameelezwa na Kaimu mganga mkuu wa serikali, Dkt. Saitor Laiza katika mkutano na wadau wa afya uliokuwa na lengo la kufahamishana juu ya matokeo ya utafiti ya ugonjwa wa kichocho uliofanywa na NIMR katika kipindi cha miaka miwili

Kaimu mganga mkuu wa serikali amesema matokeo yanaonyesha kuwa baadhi ya maeneo hapa nchini bado yanachangamoto ya ugonjwa huo hasa maeneo yanayozunguka kanda ya ziwa  huku idadi kubwa ya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakiadhirika zaidi.

"Ugonjwa wa kichocho bado ni changamoto kubwa katika maeneo ya ziwa victor,ziwa Nyasa na ziwa Tanganyika,idadi kubwa  ya watoto na watu wenye umri wa kati hadi miaka 55 waliopimwa katika Eneo la Ukerewe wameathirika katika sehemu kubwa na Tafiti kama hizi zinatuamsha sisi watekelezaji wa mifumo ya Afya na Matibabu" amesema.

Aidha, amezielekeza na kuzishauri mamlaka zinazohusika ikiwemo tamisemi  kwakuwa wao wana mamlaka makubwa kufika katika maeneo yaliyoathirika kuona namna ya kusaidia kuwatibu ilikuokoa vifo vingi ambavyo vinaweza kutokea.

"Nizishauri Mamlaka husika kama ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ndiyo watekelezaji wakubwa katika maeneo ambayo yanamadhara makubwa hata katika bajeti zetu tuzipange vizuri ili tuweze kuwaokoa watoto wasiende kuwa na madhara ya muda mrefu na pia tutaokoa vifo vingi" amesema. 

Naye Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti NIMR na mtafiti kiongozi wa mradi wa tiba, Dkt. Paul Kazyoba ameeleza s kuwa waliamua kufanya utafiti juu ya ugonjwa huo baada ya kuna haupewi kipaombele kama magonjwa mengine na kubaini kuwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaathirika Zaidi hasa katika Wilaya za Nyasa na Ukerewe.

"Katika mkutano wetu tumeangalia ukubwa wa tatizo la kichocho kwa watoto umri chini ya miaka mitano,ni moja ya Tafiti ambazo zipo kwenye Mradi wa Tiba na Matokeo yake yapo Tayari kufanyiwa Kazi ili kuondoa Tatizo la kichocho nchini" Amesema kazyoba.

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.