Na Pendo Mangala, Dodoma
Mkoa
wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa ya
Tanzania wenye postikodi namba 41000,uko katikati ya nchi na
umepakana na Mikoa ya Manyara,Morogoro,Iringa na Singida ambao pia ndio Makao
makuu ya Nchi na Serikali.
Eneo
lote la Mkoa lina jumla ya kilomita 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda
za juu kati ya mita 830 hadi 2000.
Kilimo cha Zabibu Mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo
kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya uzaidizi wa bihwana misheni,
serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha
kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya
kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine.
Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa
Afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.
Licha ya zao la Zabibu kulimwa katika maeneo mbalimbali nchini kama zao
la biashara na kuwa sehemu ya kujipatia kipato na kukuza Uchumi wa Taifa kwa
ujumla kwa wakulima wengi lakini kwa Mkoa wa Dodoma limeonekana kutia fola.
Hiyo ni kutokana
na Dodoma kubainika kuwa sehemu ya kipekee Nchini yenye sifa ya kuzalisha
zabibu zenye kiwango Cha ubora.
Stellah Hangambagi ni
Mtafiti wa kilimo kutoka Kituo Cha utafiti wa Kilimo
TARI-Makutupora anasema kuwa hali ya hewa ya Dodoma ni
nzuri na hivyo Zabibu hustawi zaidi.
Anasema sifa ya
kwanza ambayo imepelekeza Zabibu kustawi na kumea vizuri ni kutokana na Hali ya
hewa ya Dodoma ambayo inapata mvua kiasi na jua kali jambo ambalo linaipa uwezo
zabibu hiyo kuzaa Sana.
Anaitaja sifa
nyingine iliyopo Mkoani humo Zabibu inayolimwa huvunwa mara mbili
kwa Mwaka Februari na Agosti tofauti na Mikoa mingine ambayo huivuna Mara moja
tu.
"Zabibu ni fahari
ya Dodoma kwasababu Zabibu hiyo ina uwezo wa kuzaa Mara mbili kwa Mwaka na ina
ubora na mkulima anapata faida kubwa”,änasema.
Mtafiti huyo anafafanua
kuwa wamekuwa wakiongeza thamani ya mazao katika zabibu kama
kutengeneza mvinyo,kutengeneza viungo pamoja na keki.
“Kilimo cha zabibu kinahitaji
mvua za wastani japokuwa Dodoma inajulikana kwa ukame ila ardhi yake ina hifadhi
maji kwa kipindi kirefu sana kwahiyo kwa mvua zinazonyesha kuanzia Disemba
mpaka machi zinatosha kwa kuhudumia mizabibu mpaka mwezi wa julai kulekea
kipindi cha mavuno,”anasema.
Kuna aina
tatu za Zabibu ambazo ni Zabibu za mvinyo,Zabibu za mezani na Zabibu za
kukausha ambazo zote zinazalishwa Dodoma ambapo anasema Zabibu
zinazozalishwa sana Dodoma ni za mvinyo zikifuatiwa na za mezani.
Sambamba na hilo anasema
wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wakulima na wadau mbalimbali namna ya
kutumia Teknolojia kwa kuwaalika kuwapa mafunzo namna yakutumia teknoljia
kuanzia kuandaa shamba hadi kulima ili kuwa na kilimo chenye tija.
Anasema katika kipindi
cha mwaka 2020wametoa mafunzo juu ya zao hilo kwa wakulima wapatao 3500.
Mtafiti huyo
anasema katika maonesho ya nanenane wamekuwa wakitoa elimu kwa
wakulima mmoja mmoja na wadau kwa ujumla namna ya kutumia teknolojia katika zao
la zabibu.
“Kitaifa Tari makutupora
tumepewa jukumu la zao la zabibu lakini tunazalisha mazao mbalimbali ikiwemo
Mihogo Karanga na korosho hivyo tunatoa wito watu kuja kujifunza na kununua
pia,”
Wanashamba eneo la
nanaenae kumekuwa na Watafiti wakitoa mafunzo muda wote na hata wakati
wa maonyesho ya nane huku akiishukuru COSTECH kwakuwaunganisha na
waandishi wa Habari kwani wataweza kulitangaza zao hilo .
Sada Hussein ni Mratibu
wa utafiti na ubunifu anasema kituo hicho cha TARI Makutupora tayari kimetoa
kiasi Cha udongo,Mbegu za mvinyo na Teknolojia za usindikaji ikiwemo kukausha
pamoja na dawa za kunyunyuzia kwenye Mimea ya zabibu.
Anasema gharama za
uzalishaji Zabibu zinatokana na suala zima la Uendeshaji wa shamba ambapo Kuna
umwagiliaji na kutegemea mvua na wakati mkulima anaanza atapata hasara .
Pia Mkulima
ambaye anatumia mvua atawekeza milioni 10.6kwaajili ya kulima zao hilo
huku kwa mkulima anaye tumia
umwagiliaji atatumia Shilingi milioni3.
Mratibu huyo anafafanua
kuwa mkulima huyu ambaye anatumia mvua
atavuna kilo3500 kwa hekari moja kwa Mwaka na anae mwagilia
atavuna kilo 8500 kwa hekari moja.
Naye Devotha mchau toka
Idara ya uchumi kilimo anaehusika na Sayansi ya Jamii ambaye pia
anashughulikia masoko na uwekezaji kwa mkulima katika zao la Zabibu anasema kwa
Mkulima anaetegemea mvua tathmini ya haraka atavuna
wastani wa tani 4 lakini anaetumia
umwagiliaji anavuna tani10 na kuwashauri wakulima kutumia
teknojia ya umwagiliaji na kutumia teknolojia ya kisasa.
Anaeleza bei ya soko
hasa kwa Mbegu ya waine ni shilingi 1000 kwa kilo hadi
1500 lakini Zabibu za matunda kabla ya kuchakatwa ni sh3000 hadi 3500.
Hata hivyo amesema
Serikali imekuwa ikifanya tihada mbalimbali katika kuwawezesha
wakulima wadogo kwa kuanzisha mashamba darasa Kata ya Gawaye,Chinangali na
Chamwino lakini kwa Dodoma mwitikio bado mdogo kutokana na changamoto ya
utunzaji Zabibu kuwa na gharama kubwa.
Anasema kutokana na
Utafiti uliofanyika mkulima anaweza kupata ongezeko la faida hadi
asilimia 50 endapo atatumia teknolojia ya kisasa.
Naye Mkurugenzi wa
Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Makutupora,Dk.Cornel Massawe anasema wapo
katika hatua za mwisho kukamilisha utafiti wa aina tano za mbegu za Zabibu
zitakazosaidia kuongeza uzalishaji.
Massawe
anasema wanaamini Mbegu hizo zitakuwa bora zenye vigezo na
zinazotakiwa kwa mkulima ili kuongeza tija katika sekta ya kiimo ambazo
zitakuwa na uwezo wakuzalisha tani 24 kwa hekta moja.
Anazita aina hizo za
Mbegu kuwa ni Gegina,beauty,Seedless,Ruby seedless,Alphonce Lavee
na Strah ambazo zinahimili mabadiliko ya tabia nchi kama vile
ukame,mafuriko pamoja na ukame.
Aidha amebainisha kuwa
ili kuleta tija katika kilimo hicho cha Zabibu,Serikali kupitia Tume
ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH wamepokea kiasi cha Shilingi
Milioni297zitakazo tumika kuboresha kiwanda kidogo cha kuchakata zabibu.
Pia wamekuwa
wakitoa mafunzo ya ziada ya kuchakata juisi inayotokana na zabibu ili kuzuia
upotevu wa zao hilo baada ya kuvuna.
“Tumewapa wakulima elimu
ya kuchakata Zabibu lengo ni kuhakikisha wanapata tija katika kuinua
vipatao vyao,”amesema.
Mkurugenzi huyo
anaseleza kuwa baada ya wakulima kuchakata Zabibu
zao wamekuwa wanauza kwenye kiwanda ambapo asilimia 80 ya
watengenezaji wa juisi wamepata mafunzo toka TARI Makutupora.
Mwisho.
Comments
Post a Comment