Na. Netho Sichali, Afisa habari Wilaya ya Nyasa
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mh. Isabela O. chilumba,
amewataka Wajasiliamali na wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa kufanya biashara
halali, na kulipa kodi halali, pia kuacha kuingiza bidhaa kutoka nje ya Nchi na
kukwepa kulipa kodi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mh. Isabela Chilumba Akizungumza na Wajasiliamali na Wafanyabiashara Wilayani hapa kwa lengo la kujadili mambo ya msingi ya biashara Wilayani hapa. Hata hivyo amepiga marufuku ya uingizaji kiholela bidhaa toka nchi jirani ya Msumbiji na Malawi
Ameyasema hayo hivi karibuni, wakati akiongea na
wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa katika kikao cha kujadili mambo masuala ya Biashara
na maendeleo, kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Baylive uliopo Mbamba bay
Wilayani hapa.
Chilumba amefafanua kuwa, wafanyabiashara na
wajasiliamali wa Wilaya ya Nyasa wanakabiliwa na changamoto ya ukwepaji ulipaji
kodi, na kuingiza bidhaa mbalimbali, kutoka Nje ya nchi hususani, Msumbiji na Malawi kwa njia za panya ili
kukwepa kulipa kodi halali ya Serikali, na kuikosesha nchi yetu Mapato ambayo yangeweza
kujenga miundombinu ya Nchi.
Aliongeza kuwa amelazimika kuitisha kikao hicho,
ili aweze kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao, ili waweze kupata elimu ya
ulipaji kodi, na kutoa agizo la kuacha mara moja tabia ya kuingiza kiholela kwa
njia za magendo bidhaa mbalimbali kama vile mafuta ya kupikia, yanayotoka
Nchini Msumbiji na Sukari inayotoka Nchi ya Malawi.
Aidha amewataka wajasiriamali kufuata kanuni,
taratibu na sheria za kuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya Nchi kwa kukata
leseni.
“Tunachangamoto kubwa ya Wafanyabiashara wengi ya
kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka Nchi ya Msumbiji na Malawi, hasa Sukari na
Mafuta ya kupikia, ambayo huingia kwa njia isiyokuwa halali na kukwepa kulipa
Kodi. Nichukue fursa hii kuwaambia kuwa majina ya wafanyabiashara hayo tunayo
na tumekuwa tukikamata na kutaifisha pamoja na wahusika kuwachukulia hatua kali
za kisheria, lakini bado wanaendelea kufanya biashara haramu. kama Serikali
tuna wajibu wa kutoa elimu kwa Wafanyabiashara, ili wafuate Taratibu kama
tulivyoamua kuwaita kwa siku ya leo. Ili Nchi ipate mapato ni Lazima Kila mfanyabiashara
walipe kodi halali, na tutahakikisha tunawachulia hatua za kisheria, wale wote
watakaokwepa kulipa Kodi ya Serikali alisema Chilumba.
Aidha katika hatua nyingine amewapongeza wafanyabiashara
hao kwa kuchangamkia fursa za Kibiashara wilayani Nyasa kwa kuleta Bidhaa
Mbalimbali na kuhakikisha kila aina ya bidhaa inapatikana katika Wilaya ya
Nyasa hususani katika Mji wa Mbamba bay Ambao ni makao makuu ya Wilaya ya
Nyasa.
Kwa upande wao wafanyabiashara Wilayani hapa,
wameiomba Serikali ya Tanzania, kupunguza ushuru na Tozo hasa katika Bidhaa za
Nje kwa kuwa kinachosababisha wakwepe kulipa kodi ni kiwango kikubwa cha tozo wanachotozwa
na Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) hali inayowapelekea wafanyabiashara hao
kutopata faida.
Wameongeza kuwa kama Serikali itaweka viwango
rafiki vya ulipaji kodi ya Bidhaa zinazoingia toka Nchi jirani itasaidia
kufuata sheria kanuni na Taratibu za ulipaji kodi.
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Wilaya ya Nyasa
Zaitun Hamza, amewataka wafanyabiashara hao kufahamu kuwa viwango vya kodi
wanazotozwa, ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi hivyo hakuna anayeweza kupunguza
viwango hivyo vya kodi. Aidha amewahamasisha wafanyabiashara hao kununua na
kuuza bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi ili kukuza uchumi wa Nchi yetu.
MWISHO
Comments
Post a Comment