Na Jackline Kuwanda, Dodoma.
Kuelekea katika msimu wa sikuku za mwaka mpya ,Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limepiga marufuku uchomaji wa matairi barabarani .
Wito huo umetolewa leo Mkoani hapa na Kamanda wa Jeshi hilo Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa vijana waliopo mitaa ya Chang’ombe,kizota,mailimbili na kikuyu wanapaswa kuachana na mchezo huo huku akiwataka wenyeviti wa mitaa katika maeneo yao kuhakikisha kwamba hakuna uvunjifu wa amani unaofanyika .
‘’vijana hao wanaokusudia kuchoma matairi
tumesema ni marufuku kuchoma tairi barabarani kwanza wanaharibu miundombinu ya
serikali kwahiyo kama unachoma miundombinu unatualika polisi tukushughulike
kwahiyo tunawaagiza vijana hao kuachana na mchezo huo’’ Amesema Muroto
Aidha, Kamanda Muroto amewataka madereva kuzingatia
sheria za usalama barabarani huku akibainisha kuwa zipo operesheni
zinazoendelea kwaajiliya kuwakamata wale wote watakao vunja sheria.
‘’akiona anakwenda kupata kinywaji au kwenye
ulevi aache gari lake nyumbani ,akiondoka kwenda na gari kwenye ulevi ahakikishe
anakunywa kwa kiwango kinachotakiwa akizidisha kiwango akapata ajali anaanza
mwaka mbaya 2021 kwahiyo wao wachukue tahadhari ,bodabaoda pia operesheni zinaendelea
wanaopakia mishikaki ,magari,ukimbiaji wa mwendo kasi , kusimama kwenye zebra ,magari
ya serikali yanayokimbia kwa kasi yote
hayo tunazingatia kuhakikisha kwamba yanafuata sheria’’ Amesema Muroto
Hatahivyo ,Kamanda Muroto amesema Jeshi hilo kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga kuimarisha
ulinzi katika msimu huu wa sikuku za Mwaka mpya kwenye maeneo mbalimbali
ikiwemo Nyumba za Ibada ,Barabarani na kuendelea.
Mwisho.
Comments
Post a Comment