Na. Netho Sichali, NYASA
Mkuu wa wa Wilaya ya Nyasa amewataka wawekezaji wa
Utalii, kuwekeza Wilaya ya Nyasa kwa kuwa Wilaya ya Nyasa ina Vivutio Vingi vya
Utalii ambavyo, ni Vya kipekee ambavyo Vinapatikana Wilaya ya Nyasa pekee.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Isabela Chilumba akiwa katika Boti ya Uvuvi akiwa anaelekea Katika Kisiwa cha Lundo kutalii katika Tamasha la Utalii lililofanyika Nyasa Mkoano Ruvuma |
Ameyasema hayo jana wakati akihutubia wananchi alipomwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Cristina Mndeme katika Kilele cha Tamasha la Utalii
2020, lililofanyika katika Viwanja vya fisheries, Mbamba bay Wilayani Nyasa.
Mkuu huyo alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa ni Wilaya,
ya kipekee katika Mkoa wa Ruvuma, ambayo ukishindanisha na Wilaya zingine za
Mkoa wa Ruvuma, ina Vivutio vingi vizuri vinavyowavutia wageni wengi, hasa Ziwa
Nyasa na Fukwe zake za Asili ambazo zimeifanya Wilaya, hii kuwa ni ya kipekee,
na kuwataka wawekezaji kuja kuwekeza Wilaya ya Nyasa.
Aliongeza kuwa Wilaya ya Nyasa pia ina miundombinu
rafiki, ya kuwavutia watalii na Wawekezaji ukizingatia kuwa Barabara ya Mbinga hadi
Mbamba bay, Tayari imekamilika na Hospitali ya Wilaya ya Nyasa imeanza Kazi na
kutoa huduma kwa, wananchi na kuwawafanya hata watalii na wawekezaji hata wakiumwa
watatibiwa na kupata huduma bora za kiafya.
Aidha, kwa upande wa usafiri wa Maji, amewatangazia
wananchi kuwa Usafiri wa Meli ya Kisasa ya Mizigo ya Mv Mbeya 11 inaanza rasmi
kazi na jumanne wiki hii itatia Nanga katika Bandari ya Mbamba bay, na Meli ya
Mv Njombe nayo inafanya kazi.
Aidha, amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa
Juhudi zake za kuiboresha Wilaya ya Nyasa, hasa kwa miundombinu Wilaya ya Nyasa,
na sasa Hakika ni Wilaya ya Kitalii.
“Nichukue Fursa hii kumpongeza sana Mh Rais, kwa
Juhudi zake alizozifanya hasa kwa upande wa miundombinu, ametujengea barabara
ya Lami na kwa kwa sasa inapitika mwa haraka na muda wote tofauti na ilivyokuwa
mwanzo. Upande wa Usafiri wa majini Meli kubwa mbili zinafanya kazi na Mv Mbeya
imeanza kazi rasmi na Jumanne itawasili Mbamba bay hivyo, Mbamba bay imefunguka
nawakaribisha sana wawekezaji”.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ambaye
pia ni Kamishna wa Uhifadhi Tanzania National parks TANAPA, Mh. Allan Kijazi
amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuandaa Tamasha la Utalii kwa
miaka mine mfululizo, na kuwashauri kuwa wanatakiwa kuwa na Siku maalum na Tarehe maalumu ya kutangaza Vivutio vyot, na
Wizara ya Maliasili na Utalii imeyapokea maombi ya kuchangia na kuandaa Tamasha
lenye Hadhi ya Kimataifa.
Naye Mbunge Wa Jimbo
la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, ameliomba Shirika la Utangazaji Tanzania TBC,
kupitia Safari Channel Kuja kutengeneza makala na Vipindi mbalimbali vya
Vivutio vya Wilaya ya Nyasa, ambavyo ni vya aina yake kwa kuwa vivutio vingi
vya wanyama watanzania wanavifahamu sasa ni zamu ya kutangaza Ziwa Nyasa na
Fukwe zake.
Tamasha hili
limepambwa na Ngoma za Asili za Chioda, Muhambo na Lingoga, mashindano ya
kuogelea, kupiga kasia na Utalii wa Kisiwa Cha Lundo pamoja na Utali wa Nyama
choma.
MWISHO
Comments
Post a Comment