PICHA:WAZIRI JAFO NA MKURUGENZI WA KONDOA MJI WAKIWASILI ENEO LA UJENZI WA MADARASA SHULE YA SEKONDARI ULA

 


Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (wa kwanza kushoto) Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Suleman Mwogofi (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakiwasili katika eneo la ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Ula wakati wa ziara ya Mhe. Waziri.

 


Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ula wakati wa ziara yake shuleni hapo na kuwaahidi endapo watafaulu kwa daraja la kwanza mtihani wa kidato cha nne atawachagulia shule nzuri kama zawadi kwao.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.