KMC FC KUONDOKA LEO KUWAKABILI MBEYA CITY JIJINI MBEYA

Kikosi cha wachezaji 23  wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kitaondoka jioni ya leo kuelekea Jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Januari mbili katika uwanja wa Sokoine.

Aidha katika msafara huo pia utahusisha benchi la ufundi pamoja na viongozi wa tano wa Timu hiyo 

KMC FC itacheza mchezo huo wa raundi ya 18 katika mzunguko wa pili ambapo katika mzunguko wa kwanza iliweza kuifunga Timu hiyo mabao manne kwa sifuri katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Aidha kuhusu hali za wachezaji, wapo katika hali na morali nzuri itakayo wezesha kupata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kupata alama tatu muhimu ugenini dhidi ya wapinzani Mbeya City.

Hata hivyo kabla ya kuondoka, wachezaji hao wamefanya mazoezi mepesi asubuhi ya leo ikiwa ni katika mkakati wa kujiweka vizuri kuelekea kwenye mchezo huo.

Imetolewa na Christina Mwagala

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.